Wadyula (au Wadioula au Wajuula) ni kabila la jamii ya kundi la Wamandé. Kabila hilo linaishi katika nchi kadhaa za Afrika Magharibi, zikiwemo Mali, Côte d'Ivoire, Ghana na Burkina Faso.

Mkulima wa Kidyula amevaa kiremba cha kitenge cha Kidachi mnamo 1966

Hili ni tabaka la wafanyabiashara waliopata mafanikio makubwa: wahamiaji wa Dyula walianzisha jamii za kibiashara katika eneo hilo katika karne ya 14. Kwa kuwa biashara mara nyingi ilifanyika chini ya watawala wasio Waislamu, Wadyula walitengeneza seti ya misingi ya kidini kwa ajili ya Waislamu wachache katika jamii zisizo za Kiislamu. Mchango wao wa pekee katika biashara za umbali mrefu, elimu ya Kiislamu na uvumilivu wa kidini ulikuwa ni mambo muhimu katika upanuzi wa amani wa Uislamu katika Afrika Magharibi.

Marejeo

hariri

Viungo vya ne

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


  Makala hii ni sehemu ya warsha ya kuhariri Wikipedia huko MUM. Unaweza kusaidia kuihariri na kuongeza habari.
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wadyula kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.