Wagorowa

(Elekezwa kutoka Wafiome)

Wagorowa (huitwa pia Wafiome) ni kabila dogo la watu wa Tanzania ambao wanaishi katika Mkoa wa Dodoma, Wilaya ya Kondoa, na Mkoa wa Manyara karibu na mji wa Babati.

Lugha yao ni Kigorowa, moja kati ya lugha za Kikushi. Ndiyo sababu wengine wanawajumlisha na Wairaqw.

Kukadiria idadi ya watu wa Gorowa ni vigumu, kwani uhusiano wa kikabila au lugha haijarekodiwa katika sensa ya kitaifa. Idadi ya wasemaji wa Kigorowa imehesabiwa kuwa 132,748,[1] ingawa ni muhimu kutambua kwamba baadhi ya Wagorowa wanaweza kutozungumza lugha hiyo, kwa hivyo nambari hii haitalingana kabisa na idadi ya watu.

Tanbihi

hariri
  1. Harvey, Andrew (2019). "Gorwaa (Tanzania) — Language Contexts". Language Documentation and Description. 16: 127–168.
  Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wagorowa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.