Wakabras ni kati ya koo kubwa za Waluhya (jina la asili: Abaluhya) katika magharibi ya Kenya na mashariki ya Uganda. Wakabaras ni watu wanaoongea lugha ya kabila la Bantu. Wakabaras wanakaa zaidi katika kaunti ya Kakamega katika magharibi ya Kenya, lakini wanaishi katika kaunti ya Nandi na kaunti ya Uasin Gishu pia. Wao wanaishi karibu na Waisukha, Wabanyala, Watsotso, na Watachoni. Kuna Wakabaras 323.000 katika magharibi ya Kenya kutokana na hesabu zilizofanywa mwaka wa 2009.

Lugha hariri

Lugha ya zamani ya Wakabaras ni Kikabaras (jina la asili: Lukabaras, Olukabarasi, au Lukabras) na ni mojawapo ya lugha za familia ya Kiluhya; kufuatana na sensa ya Kenya ya mwaka 2009, ina wasemaji 250.000 katika Afrika Mashariki. Kufuatana na usainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie, iko nambari la E.32.

Kikabaras inafikiriwa kuendelea kuwa na kupata wasemaji zaidi. Kuna vitabu vilivyoandikwa katika Kikabaras, lakini si vingi. Kikabaras kinahusiana sana lugha ya Kitachoni, ambayo pia ni lugha mojawapo ya familia ya Kiluhya. Kikabaras haina lahaja tofautitofauti na uchunguzi haujafanywa kwa wingi kuhusu Kikabaras.

Ukoo wa Wakabaras hariri

Majina ya ukoo inatokana na majina ya wakubwa wa familia. Kuna Avatali, Abawande, Abamutama, Basonje, Abakhusia, Bamachina, Abashu, Abamutsembi, Baluu, Batobo, Bachetsi, na Bamakangala. Kati ya muungano na Waluhya wengine, wao wanafika 14% ya watu katika Kenya, wachache kwa Wakikuyu tu. Watu wakabarasi wengi sana ni wakristo, kama 90% wa umma. Watu wengi pia wanatii dini na desturi zao. Wanaume wa kabila hili wanatahiriwa, na mahari hulipwa wakati wasichana wanapoolewa.

Nyakati za Zamani hariri

Nyakati za zamani, wakabaras walikuwa wakulima wa miwa na walichunga wanyama. Kwa sababu ya kuchunga wanyama, wakabaras walihama zaidi zamani na watu wanasema kwamba wakabaras wanawez kubadilika kwa urahisi. Kabla ya ukoloni, watu wa kabaras walitii mfalmea wa Wawanga, Nabongo Mumia. Wao walikuwa na mwakilishi katika halmashauri yake. Mwakilishi wa mwisho aliitwa Soita Libukana Samaramarami. Lakini, wakati wa ukoloni, wakabaras walikuwa upande wa mabeberu, na waliwasaidia ndani ya Kenya. Kwa sababu hii, wakabaras hawakupotez viwanja vyao kama waluhya wengine ambao walipigana na mabeberu kama Wabukusu.

Watu Maarufu hariri

Katika siasa, mwanasiasa mmoja maarufu ni Dkt. Noah Mahalang'ang'a Wekesa, mbunge ya Kwanza ya zamani na waziri wa wanyama pori wakati wa ungozi wa Rais Mwai Kibaki. Pia, mwanasiasa mwingine ni Soita Shitanda. Yeye alikuwa mbunge wa eneo bunge la Malava, na waziri wa nyumba wakati wa ungozi wa Rais Mwai Kibaki. Yeye alisaidia kujenga kiwanda cha sukari cha magharibi ya Kenya katika eneo la Malava. Pia, jaji mkuu wa zamani, Zacchaeus Chesoni, alikuwa Bamachina, koo moja kati ya Wakabaras karibu na Chimoi katika eneo la Webuye.

Viungo vya nje hariri

  • http://www.ethnologue.com/show_language.asp?code=bxk
  Makala hii kuhusu utamaduni wa Kenya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wakabras kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.