Waldemar Haffkine
Waldemar Mordechai Wolff Haffkine CIE (kwa Kirusi:Мордехай-Вольф Хавкин; Odessa, 15 Machi 1860 - Lausanne, 26 Oktoba 1930) alikuwa mwanabakteriolojia ambaye alizaliwa huko milki ya Urusi lakini baadaye akawa raia wa Ufaransa.
Alihamia Ufaransa na kufanya kazi katika taasisi ya Pasteur huko Paris, ambapo alianzisha chanjo ya kipindupindu ambayo alijaribu kufanikiwa nchini India. Anatambuliwa kuwa mwanabiolojia wa kwanza aliyebuni na kutumia chanjo dhidi ya kipindupindu na tauni ya majipu. Yeye mwenyewe alichunguza chanjo hizo. Joseph Lister alimwita Waldemar "mwokozi wa ubinadamu".[1]
Tanbihi
hariri- ↑ JHALA, H. I. "W. M. W. Haffkine, Bacteriologist—A Great Savior of Mankind" (PDF). Indian Journal of History of Science.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Waldemar Haffkine kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |