Wanankhucha
Wanankhucha alikuwa nabii wa Wazigula wa Somalia aliyewaongoza katika vita vya kujitoa katika utumwa[1].
Katika vita hivyo, mawaziri wake walikuwa mzee Mwigwa na shujaa Majendero. Majendero aliuawa maeneo ya Kwamkwama na wawindaji Wabuni waliokuwa wakiishi huko. Hapo Wanankhucha alichinja ndege kama dhabihu ya kifo chake.
Kulikuwa na mtetemeko wa ardhi alipokuwa akimchinja ndege huyo, na hii ilimfanya Wanankhucha atabiri kuwa Wazigula wamefika nyumbani kwao kupya. Wengi walikubali kuendelea kuishi hapo, ingawa kulikuwa na wachache waliotaka kuendelea kugura hadi wafike walipotoka. Waliofanya hivi walizuiwa na janga lililotokea hata ikawabidi wabaki walipokuwa.
Marejeo
hariri- ↑ Bellagamba, Alice; Greene, Sandra E.; Klein, Martin A. (2013-05-13). African Voices on Slavery and the Slave Trade: Volume 1, The Sources (kwa Kiingereza). Cambridge University Press. ISBN 9780521194709.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wanankhucha kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |