Mzee ni mtu aliyeishi miaka mingi baada ya kuzaliwa.

Padri wa Kiorthodoksi, Mtskheta, Georgia.

Katika jamii za Kiafrika, sawa na jamii nyingi duniani, neno "mzee" linatumiwa pia kama cheo cha heshima kwa kumtaja mtu mwenye mamlaka fulani.

Hapo kuna hoja ya kuwa mtu aliyeendelea katika umri anawazidi vijana kwa hekima na maarifa pia, kwa hiyo anafaa kutawala au kufanya maazimio au angalau kutoa ushauri.

Mzee katika jamii

hariri

Kimapokeo tamaduni nyingi duniani zinajua heshima ya mzee. Hapo kiongozi anateuliwa kati ya wazee.

Halmashauri ya wazee ni bodi ya kufanya maazimio muhimu. Mkutano wa wazee ni mahali pa kuchukua rufaa, kwa hiyo ina kazi inayolingana na mahakama kuu katika jamii zenye taasisi hizo.

Wazee ni watu wanaotunza mila na desturi pamoja na kumbukumbu ya historia na wanapaswa kusikilizwa kwa heshima.[1]

Katika jamii zilizopangwa kwa rika (vikundi kulingana na umri), kama Wamasai au Wazulu, rika la wazee linapaswa kusikilizwa katika maazimio yanayohusu jamii yote.

Wakati umri unazidi na wazee wanakuwa dhaifu ugumu unaanza kuendelea na cheo cha heshima. Hata hivyo wote wanapaswa kuonyesha heshima kwao hata kama hali halisi hawatajali tena ushauri wao.

Tatizo hilo ni tofauti kati ya tamaduni za kimila ambako watu dhaifu hawaishi muda mrefu sana kutokana na uhaba wa nafasi za tiba upande mmoja na tamaduni zilizoendelea ambako nafasi za tiba zinawezesha watu wengi kufikia umri mkubwa ambako asilimia inaanza kupoteza akili au uwezo wote wa kutembea kwa miaka mfululizo.[2] Kama idadi ya wazee dhaifu mno inazidi ni vigumu kuendelea na hoja ya heshima kwa wazee.

Mzee katika tamaduni mbalimbali

hariri

Matumizi ya kulingana ya maneno yenye maana ya "mzee" yanapatikana kwa lugha mbalimbali:

 • "senati" katika mfumo wa kisiasa wa nchi mbalimbali ni kitengo cha bunge. Neno linatokana na lugha ya Kilatini "senatus" ambalo kiasili lilitaja "mkutano wa wazee". Katika Kilatini chenyewe neno linatokana na "Senex" yaani mtu mwenye umri mkubwa.
 • "sheikh" (‏شيخ‎) kwa Kiarabu kiasili linamtaja mtu mwenye umri wa juu; leo imekuwa neno la kutaja watawala, wakuu wa kabila fulani au pia viongozi wa makundi ya kidini ya Kiislamu.
 • neno "kuhani" katika lugha nyingi (kwa mfano "priest" kwa Kiingereza) linatokana na lile la Kigiriki πρεσβύτερος, presbýteros, lenye maana asili ya "mzee".

Tanbihi

hariri
 1. Elders were and are the guardians of the culture, traditions, and history of the people. Integrity, generosity, wisdom, articulateness, subtlety, patience, tactfulness, gratefulness, and being listened to and respected by others are all qualities of an Elder. Elder Roles
 2. "Culture and the Meaning of a Good Old Age" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2015-11-29. Iliwekwa mnamo 2015-04-15.

Marejeo

hariri
 • Bishop, Jonathan. Examining the Concepts, Issues, and Implications of Internet Trolling. IGI Global. Hershey, PA. 2013.
 • Bolen, Jean Shinoda Crones Don’t Whine. Conari Press. Boston. 2003.
 • Gutmann, David. Reclaimed Powers. Northwestern U. Press. Evanston, Ill.1994
 • Dass, Ram. Still Here.Embracing Aging, Changing, and Dying .Riverhead Books.New York. 2001.
 • Jones, Terry. Elder: A spiritual alternative to being elderly. Elderhood Institute. 2006.
 • Jones, Terry. The Elder Within: Source of Mature Masculinity. Elderhood Institute. 2001.
 • Leder, Drew. Spiritual Passages. Jeremy P. Tarcher/Putnam. New York. 1997.
 • Levinson, Daniel J. The Seasons of a Man’s Life. Ballantine Books. NY. 1978.
 • Raines, Robert. A Time to Live. Seven Steps in Creative Aging. A Plume Book. New York. 1997.
 • Schachter-Shalomi, Zalman. Ageing to Sageing. Warner Books. N.Y. 1995.