Mpumalanga
Mji Mkuu | Nelspruit |
’‘‘Mji Mkubwa’’’ | Nelspruit |
Waziri Mkuu | Thabang Makwetla (ANC) |
Eneo |
Nafasi ya 8 kati ya majimbo ya Afrika Kusini |
- Jumla | 79 490 km² |
Wakazi | Nafasi ya 5 kati ya majimbo ya Afrika Kusini |
- Jumla (2001) | 3 122 994 |
- Msongamano wa watu / km² | 39/km² |
Lugha | SiSwati (30.8%) IsiZulu (26.4%) IsiNdebele (12.1%) Sepedi (10.8%) |
Wakazi kimbari | Waafrika Weusi(92.4%) Wazungu (6.5%) Chotara(0.2%) Wenye asili ya Asia (0.2%) |
Mpumalanga (kabla ya 2002 iliitwa Eastern Transvaal) ni moja kati ya majimbo 9 za Afrika Kusini. Kuna wakazi 3,364,000 (2001) kwenye eno la 79,512 km². Jimbo lilianzishwa mwaka 1994 kutokana na sehemu za jimbo la awali la Transvaal na maeneo ya bantustan KaNgwane, KwaNdebele na Lebowa. Mji mkuu ni Nelspruit.
Neno Mpumalanga limetokana katika lugha ya Kiswazi likimaanisha "mahali pa macheo".
Jiografia
haririMpumalanga imepakana na Eswatini na Msumbiji halafu na majimbo ya KwaZulu-Natal, Dola Huru, Gauteng na Limpopo. Hifadhi ya Kruger ambayo ni hifadhi ya wanyama mashuhuri imo jimboni.
Kuna kanda mbili za tambarare za juu penye usimbishaji kidogo na tambarare za duni penye mvua nyingi.
Uchumi
haririKilimo
haririSehemu kubwa ya eneo hutumiwa kwa kilimo. Mazao ni pamoja na mahindi, ngano, ntama, alizeti, soya, karanga, miwa, mboga, kahawa, chai, pamba, tumbako, machungwa na matgunda mengine.
Misitu huvunwa hasa katika kaskazini penye kiwanda kikubwa cha karatasi cha Ngodwana.
Takriban 14% za eneo hutumiwa kwa mifugo hasa ng'ombe na kondoo.
Migodi
haririKati ya madini yanayochimbwa ni: dhahabu, platini, shabha, makaa mawe na mengi mengine.
Mpumalanga huzalisha 83% za makaa mawe ya Afrika Kusini.
Utalii
haririHifadhi ya Kruger ina eneo la 20,000 km² hutembelewa sana na watalii.
Viungo vya nje
hariri
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mpumalanga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |