Wanjiru Kihoro

Wanjiru Kihoro (1953 - 12 Oktoba 2006) alikuwa mwandishi na mwanaharakati wa kike kutoka nchini Kenya. Alikuwa kati ya waanzilishaji wa chama cha Akina Mama wa Afrika (AMwA) na Kamati kwa uhuru wa wafungwa wa kisiasa wa Kenya iliyopinga kufungwa kwa Wakenya wakati wa serikali ya Daniel arap Moi[1][2]

Elimu na kaziEdit

Alizaliwa Nyeri, Kenya akamaliza elimu ya sekondari kwenye Kenya High School huko Nairobi. Kihoro alisoma uchumi kwenye Columbia University, New York. Akachukua MA ya Development Studies na PhD kwenye Chuo kikuu cha Leeds (Uingereza) wakati wa miaka ya 1980.[1][2]

Alifunga ndoa na Wanyiri Kihoro wakawa na watoto wanne Wangui, Pambana, Amandla and Wairimu.

Mnamo 1982 Kihoro na mumewe walihamia London wakati serikali ya Arap Moi ilizidi kukamata na kufunga wapinzani nchini. Hapa alishiriki kuanzisha Kamati kwa uhuru wa wafungwa wa kisiasa wa Kenya. Alifanya kazi kwa The Africa Centre, London mwaka 1984 na baadaye kwa All African Conference of Churches na National Christian Council of Kenya na United Church Board for World Ministries.[1][2]

Mwaka 1985 alishiriki kuunda Akina Mama wa Afrika , halafu mwaka 1992 taasisi ya ABANTU for Development inayolenga kufundisha wanawake wa Kiafrika kwa nafasi za uongozi.[3]

2002 baada ya uchaguzi wa Mwai Kibaki alirudi Kenya.[1][2]

KifoEdit

Mwaka 2002 alipata ajali ya ndege akakaa katika hali ya kuzimia kwa muda wa miaka minne akaaga dunia mwaka 2006. [4]

Baada ya kifo chake gazeti la The Guardian ikaandika ya kwamba "Wanawake wachache wa afrika wamajulikana vema kama Wanjiru Kihoro".[1] Wangui wa Goro aliandika: "alikuwa kiongozi, mwanaharakati kwa demokrasia, uhuru, haki za binadamu, usawa na haki akawa daima kwa upande wa wakereketwa hasa wanawake na maskini. Alichapa kazi bila kuchoka na kwa ujasiri."[5]

marejeoEdit

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 Haward, Patricia. "Wanjiru Kihoro", 22 November 2006. Retrieved on 23 August 2014. 
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 Wanjiru Kihoro: an activist, feminist, patriot, visionary, leader, friend. Pambazuka News www.pambazuka.org (19 October 2006). Iliwekwa mnamo 23 August 2014.
  3. Partner in Focus. Women's Environment and Development Organization www.wedo.org. Iliwekwa mnamo 15 September 2014.
  4. Telewa, Muliro. "Meeting 'Kenya's Terri Schiavo'", 6 April 2005. Retrieved on 23 August 2014. 
  5. wa Goro, Wangui (19 October 2006). Wanjiru Kihoro: Sister, Comrade, Friend. Pambazuka News www.pambazuka.org. Iliwekwa mnamo 24 August 2014.

Viungo vya NjeEdit