Daniel Arap Moi

(Elekezwa kutoka Daniel arap Moi)

Daniel Toroitich arap Moi (2 Septemba 1924 - 4 Februari 2020) alikuwa Rais wa Kenya kutoka mwaka 1978 mpaka 2002.

Daniel Toroitich arap Moi


Muda wa Utawala
22 Agosti 1978 – 30 Desemba 2002
Makamu wa Rais Mwai Kibaki (1978–1988)
Josephat Karanja (1988–1989)
George Saitoti (1989–1998, 1999-2002)
Musalia Mudavadi (2002)
mtangulizi Jomo Kenyatta
aliyemfuata Mwai Kibaki

tarehe ya kuzaliwa 2 Septemba 1924 (1924-09-02) (umri 100)
Sacho, Kenya Colony
tarehe ya kufa 4 Februari 2020
chama Kenyan African National Union (KANU)
chamakingine Kenya African Democratic Union (KADU) (1960–1964)
ndoa Lena Moi (d. 2004)
signature Daniel arap Moi

Maisha na mwanzo wa siasa

Moi alizaliwa Sacho, wilaya ya Baringo, Mkoa wa Bonde la Ufa, na alilelewa na mama yake Kimoi Chebii, kufuatia kuaga dunia mapema kwa baba yake.

Baada ya kumaliza masomo ya chuo cha upili cha Tambach, aliweza kujiunga na chuo cha ualimu mjini Kapsabet.

Alifanya kazi kama mwalimu kutoka mwaka 1946 hadi 1955.

Mwaka wa 1955 Moi aliingia siasa akachaguliwa kwa kiti cha wanabaraza wa mkoa wa bonde la ufa.

Mwaka wa 1960, Moi na Ronald Ngala waliunda chama cha KADU ambayo kwa Kiswahili ni Muungano wa Demokrasia ya Waafrika wa Kenya kilichoshindana na KANU iliyoongozwa na Jomo Kenyatta. Lengo la KADU, lilikuwa kuhifadhi maslahi ya makabila madogo kama Wakalenjin dhidi ya makabila makubwa kama Waluo na Wakikuyu, makabila ambayo yalikuwa zaidi upande wa chama cha KANU, Kenyatta mwenyewe akiwa Mkikuyu.

KADU ilipendelea katiba ya majimbo ambapo mamlaka nyingi zingebaki kwenye ngazi za chini, na KANU ilipendelea mfumo wa serikali ya umoja ambapo mamlaka zingeunganishwa mikononi mwa serikali ya kitaifa. KANU ilipata kura nyingi katika uchaguzi kabla ya uhuru, hivyo serikali ya kikoloni ya Waingereza iliachana na katiba ya majimbo.

Mwaka wa 1957, Moi alichaguliwa kwa baraza la Bonde la Ufa tena, na mwaka wa 1961 kwa baraza la bunge kwa kiti cha Baringo ya Kaskazini.

Baadaye akawa Waziri wa Elimu mwaka wa 1960–1961, bado kabla ya uhuru wa Kenya.

Makamu wa rais

Baada ya Kenya kupata uhuru mnamo 12 Desemba 1963, Kenyatta alimsihi Moi ya kwamba KADU na KANU ziungane pamoja kumaliza ukoloni. Kwa hiyo Kenya ikawa nchi ya chama kimoja, ikiimarishwa na muungano wa wengi Wakĩkũyũ-Waluo.

Moi, aliweza kupanda cheo na kuwa waziri wa mambo ya ndani mwaka 1964, hasa kwa umuhimu wake kuleta faraja za watu wa bonde la ufa na jumla KADU kwa serikali ya umoja wa Taifa.

Baadaye aliweza kupanda cheo zaidi akawa Makamu wa Rais mnamo 1967. Kama kiongozi kutoka kabila dogo, alituliza makabila haya makubwa nchini Kenya.

Lakini, Moi alipingwa na wanasiasa wa makabila makubwakubwa, hasa Wakikuyu na Waluo. Walijaribu kubadilisha katiba na kufuta kanuni iliyomfanya makamu wa rais kuchukua nafasi yake wakati rais anaaga dunia. Hata kwa uzee na afya yake Kenyatta kudhoofika, alipinga mipango hii; katiba ilibaki jinsi ilivyokuwa.

Urais wa Moi

Mzee Jomo Kenyatta alipoaga dunia tarehe 22 Agosti 1978, Moi alichukua kiapo na kuwa Rais wa Kenya. Alikuwa na sifa nchini, kona zote. Alisafiri sehemu na maeneo yote Kenya, na basi wananchi wakampa faraja na hongera. Alipochukua kiapo kuwa Rais wa Kenya, alinena kwamba atafuata "nyayo" za Mzee Kenyatta, kwa maana ataendelea na sera za Kenyatta na umoja wa Harambee. Ijapokua wapinzani wake wa kisiasa, hasa kutoka makabila makubwa, walimwona Moi kama rais wa mpito tu, asiyeweza kukaa muda mrefu kwa sababu ametoka katika kabila dogo.

Mnamo 1 Agosti 1982, kundi la askari wa jeshi la anga la Kenya, wakiongozwa na Hezekiah Ochuka, lilijaribu kumpindua Moi, lakini walikuta upinzani wa mikono mingine ya jeshi na polisi waliosimama upande wa rais na kushinda uasi (Ona uasi wa wanahewa wa Kenya 1982).

Moi alichukua fursa hiyo kuwafukuza wapinzani wa kisiasa na kuimarisha nguvu yake. Alipunguza ushawishi wa wafuasi wa Kenyatta kwenye baraza la mawaziri kupitia uchunguzi wa muda mrefu. Uchunguzi huo ulionyesha kwamba wanasiasa kadhaa walikuwa wakishiriki katika uasi. Moi aliwasamehe lakini alifaulu kuwaonyesha kama wasaliti mbele ya jamii ya Kenya. Viongozi wa uasi huo, pamoja na Ochuka walihukumiwa kufa, na hii ilikuwa mara ya mwisho hukumu za mauti zilitekelezwa Kenya [1]. Moi alipandisha ngazi wafuasi wake waaminifu, akabadilisha katiba kuifanya KANU iwe chama cha kisiasa pekee kinachoruhusiwa kisheria nchini. Wasomi wengi hawakukubali mabadiliko hayo walimoona mwelekeo wa kidikteta. Vyuo vikuu vilikuwa chanzo cha harakati ambazo zilitaka kuanzisha mageuzi ya kidemokrasia. Walakini, polisi jasusi iliingilia vikundi hivyo na wanaharakati wengi wa demokrasia walikwenda uhamishoni. Serikali ilipiga marufuku kufundishwa kwa Umarx katika vyuo vikuu vya Kenya. Harakati za siri zilizaliwa, kama vile Mwakenya na Pambana. [2]

Moi, alijulikana ng'ambo kama kiongozi anayeunga mkono Ulaya ya magharibi, kwa vita baridi kati ya Ukomunisti na Ukapitalisti. Kenya ilikuwa kwa Muandamano wa kutojiunga. Lakini serikali za Ulaya ya magharibi ziliona Kenya kama nchi inayopinga Ukomunisti na hivyo kambi ya nguvu kwao kushinda ukomunisti. Kwa hiyo Kenya ilipokea misaada kutoka nchi za kibepari zaidi ili kuzuia ujamaa uliotambakaa, Ethiopia, Somalia, Tanzania na pia Vita za Uganda. Kwa hiyo siasa za uhuru na haki za kibinadamu, hazikuwazisha Ulaya ya magharibi hata kidogo.

Lakini, vita baridi vilipokwisha kwa kuanguka kwa Umoja wa Kisovyeti, mambo hayo mapya yakatokea, mwandamano wa watu na wanasiasa kuitisha demokrasia ya vyama nyingi, wakiongozwa na Matiba na Oginga Odinga. Moi alianza kuonekana kama mdhalimu kwa sababu alianza kuwafunga jela wanamgambo wa kidemokrasia, na pia jela nyingine za kisiri ambazo watu waliteswa kwa kunanuliwa na swali. Ulaya ya Magharibi ikaacha kuipa Kenya usaidizi wa kigeni na kwa kazo pande zote ndani ya Kenya na ng'ambo, Moi kakubali kuruhusu Demokrasia ya vyama nyingi, ambapo Moi mwenyewe kaunga uchaguzi na kukampaini kwa nguvu zaidi kwa kupinga upinzani Kasarani mnamo Desemba 1991.

Moi alishinda uchaguzi wa miaka 1992 na 1997, ambapo ulizidi kwa vita vya ukabila mkoa wa bonde la ufa. Moi aliweza kuwagawa watu wa upinzani kwa kukema ukabila, na vyama vya upinzani kupasuka kwa kambi za faraja za kabila. Pia inasemekana wizi wa kura, hasa mkoa wa bonde la ufa na Ukambani.

Ufisadi serikalini

Mwaka wa 1999 Intidhamu zisizohusika na serikali kama Amnesty [1] na uchunguzi wa Umoja wa Mataifa [2] zilichapishwa kuonyesha haki za kibinadamu kwa wapizani wa siasa hazikutetewa Kenya Moi akiwa Rais.

Jina la Moi lilitajwa kwa Ufisadi wa 'migodi' na uzuiaji wa ufisadi huo, ambapo serikali kwa sahihi za watu wachache ilisemekana imetoa pesa ya kununua na kuuza migodi ng'ambo kwa jina la kampuni bandia Goldenbarg ambapo Kamlesh Pattni, mfanyabiashara wa Kenya, alisemekana kuwa fisadi halisi kwa oparesheni za Goldenbarg na wanasiasa waliohusika. Ilisemekana kwamba Moi aliiona Goldenberg kama njia ya kupata pesa za kigeni nchini Kenya ambapo uchumi, utalii na usaidizi wa kigeni ulipokoma mwaka wa 1992. Hivyo goldenberg ilinunua na kuuza migodi iliyochomolewa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo. Aibu hii ya Goldenbarg ni gharama ya asilimia 10 ya utolezi wa uchumi mwaka mmoja.

Pesa zilizolipwa Goldenbarg, zilikuwa zitolee kenya pesa za kigeni lakini kwa sababu ni mambo fisadi, basi waliopewa pesa hizo wakurudisha na basi serikali ya Mwai Kibaki ilijaribu kuchunguza kesi yenyewe zaidi.

Kung'atuka

Rais Moi, kazuiwa na katiba kwa Uchaguzi wa mwaka 2002. Wengi kwa faraja za Moi walisema katiba itekelezwe ili achaguliwe mara ya tatu, lakini Moi mwenyewe kawapinga na kutawa, na kumchagua Uhuru Kenyatta, mwana wa Rais wa kwanza, kama mwenyekiti kwa chama cha KANU. Raila Amollo Odinga kwa bidii, alikampainia Mwai Kibaki, ambaye alishinda urais kwa muungano wa NARC na Kukiriwa 29 Desemba 2002.

Moi aliishi kwa utawa mjini Kapsabet, ambapo huduma zake za amani na usaidizi azifanyia kwa Chuo cha Moi Afrika. Wakenya wengi wamtambua Moi kwa hoja na vigelegele mahali popote aliposimama. Moi aliunga nchi ya umoja, ambayo inaunganisha makabila yote, juzi siku ya uchaguzi wa maono wa katiba mpya, Moi kaipinga katiba ambayo itagawa watu. Katiba mpya ilipokataliwa na watu, Kibaki kwa hadhara, yasemekana na magazeti kwamba kapanga mkutano na Moi kujadili njia ya kusonga mbele.

Tazama pia

Tanbihi

  1. Joseph Ndunda. "No hanging since 1987: Is death penalty still relevant?", The Star, 7 September 2016. 
  2. Stephen Mburu. "Govt reaction was very harsh", 12 March 2000. Retrieved on 2020-02-05. Archived from the original on 2020-02-04.