Waruhiu Itote
Waruhiu Itote (General China; 1922 - 30 Aprili 1993) alikuwa mmoja wa viongozi muhimu wa uasi wa Mau Mau akiwa pamoja na Field Marshal Dedan Kimathi, Generali Stanley Mathenge na Field Marshal Musa Mwariama.
Itote alitiwa baloni na vikosi vya jeshi la Uingereza hapo 15 Januari 1954, lakini tofauti na Kimathi, hatimaye aliachiliwa huru.
Mwakani 1967 Itote alichapisha tawasifu yake, " 'Mau Mau' General" (East African Publishing House), na mwakani 1979 aliandika "Mau Mau in Action" (TransAfrica Books).
Alihudumu kama afisa wa juu wa huduma ya Kenya National Youth Service katika afisi zao kuu Ruaraka, Nairobi.
Itote alizaliwa katika kijiji cha Kaheti, taarafa ya Mukurwe-ini, Wilaya ya Nyeri hapo mwaka wa 1922.
Alikufa ugonjwa wa kiharusi hapo mwaka mwaka wa 1993 akiwa na umri wa miaka 71. Wakati wa kifo chake alikuwa akisimamia shamba, karibu na Ol Kalou.
Viungo vya nje
hariri- Tawasifu ya Nje
- Daudi Blumenkrantz "He Deserved a State Burial" Ilihifadhiwa 28 Februari 2007 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Waruhiu Itote kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |