Washeli[1] (ing. washer) ni kisahani chembamba (kawaida kina umbo la duara, wakati mwingine ni la mraba) chenye tundu katikati. Hutumiwa pamoja na bolti na nati.

Washeli mbalimbali: bapa, kugawanyika, kinyota na kihami

Kazi yake ni hasa kutandaza mkazo kwenye uso mkubwa zaidi wa kitu kinachoshikiliwa. Washeli hutumiwa pia kuongeza umbali wakati wa kuunganisha vitu viwili.

Ni muhimu pia kwa kutenganisha dutu tofauti kama alumini na feleji ya bolti / nati inayoweza kusababisha ulikaji.

Washeli kwa kawaida hutengenezwa kwa metali au plastiki. Zile za mpira au plastiki hupunguza mitikisiko.

Washeli zenye uso wa meno huongeza mshiko baina ya nati na bolti na kuzuia kufunkuka kwa mshiko.

Washeli bapa pamoja na washeli ya pili ya springi huwekwa kwenye bolti kati ya nati (kwenye ncha iliyofungwa) na kichwa cha bolt.

Marejeo hariri

  1. "Washeli" ni msamiati kutoka Kamusi ya TUKI-ESD; kamusi nyingine hazina neno la Kiswahili kwa jambo linalotajwa.

Viungo vya nje hariri