"Watora Mari" ni jina la wimbo ulitoka tarehe 12 Agosti 2016 ambao umetungwa na kuimbwa na mwimbaji wa Kizimbabwe, Jah Prayzah. Wimbo umemshirikisha msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania, Diamond Platnumz. Ni moja kati ya nyimbo za Jah Prayzah zilizopata mafanikio makubwa sana. Wimbo umepata kutazamwa mara milioni 1 ndani ya masaa 18 katika Youtube.[1] Unaufanya kuwa wimbo wa pili kutazamwa sana kwa wasanii kutoka nchini Zimbabwe baada ya Hello (wimbo wa Adele ameuimba tena) ya Taps Mugadza.[2][3] Vilvile unakuwa wimbo wa kwanza wa Diamond kuimba na watu wa Zimbabwe na vilevile wa kwanza kwa msanii yeyote kutoka Tanzania kushirikiana na watu wa Zimbabwe.[4] Diamond humu anaimba baadhi ya maneno ya Kishona.

“Watora Mari”
“Watora Mari” cover
Picha ya kiwambo cha video ya Watora Mari
Single ya Jah Prayzah akiwa na Diamond Platnumz
kutoka katika albamu ya Mdhara Vachauya
Imetolewa 12 Agosti, 2016
Imerekodiwa 2016
Aina Bongo Flava, muziki wa Zimbabwe
Urefu 3:48
Studio Wasafi Records
Mtunzi Jah Prayzah
Diamond Platnumz
Mtayarishaji Laizer Classic
Mwenendo wa single za Jah Prayzah akiwa na Diamond Platnumz
"Chinamira"
(2015)
"Watora Mari"
(2016)
"Mdhara Vachauya"
(2016)

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri

Viungo vya Nje

hariri