Watu weusi

Watu weusi mara nyingi humaanisha watu kutoka Kusini kwa Sahara, ingawa rangi hiyo ya ngozi (nyeusi ama ya kahawia) inatawala katika maeneo mengine mengi ya dunia, kuanzia India kusini hadi Australia, mbali na watu wenye asili ya Afrika waliohamishwa au waliohama, hasa kwenda Amerika, tangu karne ya 16.

Pamoja na hayo, wengi wanaona msamiati huo si sahihi wala haina adabu, kwa jinsi unavyotumika.