Wikipedia:Makala ya wiki/Kassim Mapili
Kassim Said Mapili (1937 - 2016) alikuwa mwanamuziki maarufu wa muziki wa dansi kutoka nchini Tanzania. Mzee Mapili alizaliwa katika kijiji cha Lipuyu, Tarafa ya Lionya, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi mwaka 1937. Hivyo umauti umekuta Mzee Mapili akiwa na umri wa miaka 79. Alipata elimu ya msingi huko kwao Lipuyu, sambamba na kupata elimu ya dini na mwenyewe aliwahi kusema alianza kupata mapenzi ya kuimba wakati alipokuwa Madrasa akighani Kaswida. Mwaka 1958 alijiunga na White Jazz Band iliyokuwa na masikani yake huko Lindi.
Mwaka mmoja baadaye akahamia Mtwara na kujiunga na Mtwara Jazz Band, lakini mwaka 1962 akajiunga na Honolulu Jazz Band ambayo nayo ilikuwa hapo hapo Mtwara. Mwaka 1963, Mzee Mapili akachukuliwa na TANU Youth League ya mjini Lindi, na kujiunga na bendi ya Jamhuri Jazz Band ya hapo Lindi. Mwaka 1964 Mzee Mapili akachaguliwa kuanzisha bendi ya TANU Youth League ya Tunduru. Mwaka mmoja baadaye alihamia Kilwa Masoko na kujiunga na Lucky Star Jazz Band ya mji huo. ►Soma zaidi