Wikipedia:Makala ya wiki/Umaru Yar'Adua
Umaru Musa Yar'Adua (16 Agosti 1951 – 5 Mei 2010) alikuwa mwanasiasa kutoka nchini Nigeria na rais wa nchi hiyo tangu 2007 hadi kifo chake hapo 2010. Yar'Adua ni Mwislamu aliyezaliwa katika familia ya Wafulbe katika Nigeria ya Kaskazini. Babake Musa Yar'Adua alikuwa waziri katika serikali ya kwanza ya nchi baada ya uhuru. Kakaye jenerali Shehu Musa Yar'Adua alikuwa makamu wa rais chini ya Olusegun Obasanjo kati ya 1976 hadi 1979 akafungwa jela chini ya udikteta wa Sani Abacha.
Umaru Yar'Adua alisoma kemia tangu 1972 kwenye chuo kikuu cha Ahmadu Bello mjini Zaria akawa mwalimu kwenye vyuo mbalimbali. Tangu 1983 akaacha mafundisho akijishughulisha na makampuni mbalimbali. 1999 baada ya serikali ya Abacha alichaguliwa kuwa gavana wa jimbo la Katsina akarudishwa mwaka 2003.
Yar'Adua alisifiwa kwa sababu alitangaza mali yake kabla ya uchaguzi 1999 und 2003. Anasemekana alikuwa gavana aliyekataa rushwa. Aliykuwa kati ya magavana wachache wasiochunguliwa na mamlaka ya kupambana na rushwa "Economic and Financial Crimes Commission". ►Soma zaidi