Wikipedia:Mwongozo (Kuhariri)

Utangulizi   Kuhariri   Kuanzisha Makala   Muundo   Viungo vya Wikipedia   Kutaja vyanzo   Kurasa za majadiliano   Kumbuka   Kujisajili    
Bonyeza "hariri chanzo" kubadili makala
Bonyeza "hariri chanzo" kubadili makala

Ukurasa huu unaeleza hali ya kihariri cha kawaida (wiki-text-editor). Kwa kutumia kihariri oneshi (VisualEditor) bofya hapa (ukiona maandishi mekundu, maana yake ni kwamba haijaandaliwa).

Unaweza kuhariri kila ukurasa wa Wikipedia yaani kusahihisha, kuongeza habari, kuziondoa au kuzibadilisha. Karibu kila ukurasa una kiungo kinachosema "hariri chanzo", ambacho kinakupatia nafasi ya kubadilisha ukurasa unaotazama. (Kurasa chache zinalindwa hazikupi nafasi hii.)

Hiki ni kipengele muhimu sana cha Wikipedia, na wote wanaruhusiwa kuhariri. Iwapo unaongeza habari fulani kwenye makala, tafadhali weka marejeo, kwa sababu habari zisizo na uthibitisho kuna uwezekano mkubwa wa kuondolewa. Pia ni ushauri mwema kwamba kutafuta majadiliano kwenye ukurasa wa majadiliano kama unataka kuleta mabadiliko makubwa hasa ukiona mwandishi aliyetangulia alikosea na wewe unatarajia kuleta habari za kinyume. Kujadiliana kwanza inasaidia kuepukana na vita ya uhariri.

Nenda kwenye sanduku la mchanga na ubonyeze kiungo cha "hariri chanzo". Hii itafungua dirisha la kuhariria lililo na maandishi ya ukurasa huu. Weka kitu cha kujifurahisha au "Salam ulimwengu!", halafu Hifadhi kurasa na tazama nini ulichokifanya! Kuwa mwangalifu kuhakikisha kwamba unahariri ukurasa wa sanduku la mchanga, si maandishi ya ukurasa huu wa mwongozo.

Onyesha hakikisho

Moja ya kipengele muhimu cha kuanza kutumia sasa ni kitufe cha Onyesha hakikisho la mabadiliko. Jaribu kufanya uhariri kwenye sanduku la mchanga, halafu bonyeza kitufe cha Onyesha hakikisho la mabadiliko badala ya Hifadhi Kurasa. Hii inakuruhusu kuona kurasa itakavyoonekana baada ya kuhifadhi, kabla hujahifadhi. Wote twafanya makosa; kipengele hiki kinakuonyesha makosa hayo. Kutumia Onyesha Hakikisho la Mabadiliko kabla ya kuhifadhi pia inakuruhusu kujaribu kubadili miundo na maharirio mengine bila ya kupagaranyua historia ya kurasa. Usisahau kuhifadhi maharirio yako baada ya kuhakiki!

Kitufe cha "Onyesha hakikisho la mabadiliko" kipo upande wa kulia baada ya kitufe cha "hifadhi kurasa" na chini yake ni uga ya "kuhariri muhtasari.

Muhtasari wa kuhariri

Kabla hujagonga Hifadhi kurasa ni adabu nzuri kuingiza maelezo mafupi sana kuhusu kile ulichobadilisha kwenye sanduku la Muhtasari lililopo baina ya dirisha la kuhariria na kitufe cha Hifadhi kurasa. Inaweza kuwa kifupi sana; kwa mfano kama unaingiza neno "typo", watu watajua kama umefanya masahihisho ya tahajia. Pia, iwapo mabadiliko uliyoyafanya kwenye kurasa yalikuwa madogo, kama vile kusahihisha tahajia na makosa ya kisarufi, kuwa makini kutazama kisanduku cha "Haya ni mabadiliko madogo" (hii inapatikana ukiwa umeingia kwenye akaunti yako tu, basi).

Kufuatilia kazi yako

Kitufe cha "Kufuatilia" kipo juu ya makala upande wa kulia kabisa; kitufe cha "maangalizi yangu" kiko juu ya kila dirisha.

Labda unapenda kuangalia makala ulipochangia kwa njia ya kuhariri au makala uliyoanzisha inaendelea jinsi gani kwa njia ya michango ya wengine. Hapa unaweza kubofya juu ya makala inaposema "Fuatilia". Ukiwa mwanawikipedia aliyejiandikisha makala hii imeingizwa sasa katika orodha yako ya maangalizi. Orodha hii naweza kutazama ukibofya "maangalizi yangu" na kibonye hiki kiko juu kabisa kwenye kila ukurasa wa wikipedia.


Jaribu kuhariri katika sanduku la mchanga
Endelea mwongozo na Kuanzisha Makala