Wikipedia ya Kihispania
Wikipedia ya Kihispania (Kihispania: Wikipedia en Español) ni toleo la kamusi elezo ya Wikipedia kwa lugha ya Kihispania. Ilianzishwa mnamo mwezi Mei, 2001. Mnamo tar. 8 Machi ya mwaka wa 2006, Wikipedia ya Kihispania imefikisha makala 100,000.
Kwa sasa, ni Wikipedia ya 9 kwa ukubwa kwa hesabu ya makala, inafuatiwa na Wikipedia ya Kisweden mnamo mwezi Aprili 2007. Zamani ilikuwa Wikipedia ya 8 kwa ukubwa, hadi ilipofika mwezi wa Mei mwaka 2005 ikapitwa na Wikipedia ya Kireno kisha Wikipedia ya Kiitalia kunako mwezi wa Agosti 2005. Mnamo tar. 18 Novemba 2007, Wikipedia ya Kihispania imefikisha makala 300,000.
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- (Kihispania) Spanish Wikipedia
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wikipedia ya Kihispania kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |