Wilaya ya Bumbuli ni kati ya wilaya 11 za Mkoa wa Tanga[1][2] nchini Tanzania. Wilaya ya Bumbuli kwa upande wa kaskazini imepakana na wilaya ya Lushoto; pia imezungukwa mara tatu kwa upande wa kusini na wilaya ya Korogwe. Ilitenganishwa kutoka wilaya ya Lushoto mnamo mwaka 2013.

Ramani ya mahali pa wilaya ya Bumbuli, pamoja na Lushoto katika Mkoa wa Tanga

Wilaya ya Bumbuli mnamo mwaka 2016 iligawanywa kiutawala kwa mitaa kumi na nane.

Mwaka 2015 ilikadiria kuwa na wakazi 174,938 [3] walioishi katika wilaya hiyo. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 159,373 [4].

Wilaya ya Bumbuli ilitengwa kwenye mwaka 2015 na Wilaya ya Lushoto[5][6]. Iko kwenye kitovu cha milima ya Usambara. Ujenzi wa ofisi kuu ya wilaya ulianzishwa kenye kijiji cha Kwehangala, kata ya Dule B[7]. Mwaka 2019 mwenyekiti wa kamati ya bunge alisema kwamba wilaya hiyo ilikuwa hatarini ya kufutwa tena kwa sababu ilishindwa kukusanya mapato ya kutosha[8]

Wakazi asilia ni hasa Wasambaa.

Marejeo hariri

  1. https://www.nbs.go.tz/nbs/takwimu/majimbo/MAJIMBOApril_Kisw.pdf
  2. https://zabuni.co.tz/storage/tenders/1611390088.pdf
  3. Makadirio ya Idadi ya Watu katika Majimbo ya Uchaguzi kwa Mwaka 2016, Tanzania Bara. April, 2016, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Wizara ya Fedha na Mipango, Dar es Salaam
  4. https://www.nbs.go.tz
  5. https://lushotodc.go.tz/storage/app/uploads/public/5a0/b0a/548/5a0b0a5485966968107954.pdf
  6. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-12-27. Iliwekwa mnamo 2023-05-14. 
  7. Makao makuu halmashauri ya Bumbuli kujengwa Kwehangala, tovuti ya maendeleovijiini.blogspot ya tarehe 25.05.2018, iliangaliwa Oktoba 2020
  8. Halmashauri Bumbuli hatarini kufutwa Archived 9 Oktoba 2020 at the Wayback Machine., Gazeti ya Habarileo ya tar. 272.08.2029, iliangaliwa Oktoba 2020

Viungo vya Nje hariri

  Kata za Wilaya ya Bumbuli - Mkoa wa Tanga - Tanzania  

Baga | Bumbuli | Dule "B" | Funta | Kisiwani | Kwemkomole | Mahezangulu | Mamba | Mayo | Mbuzii | Mgwashi | Milingano | Mponde | Nkongoi | Soni | Tamota | Usambara | Vuga


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Bumbuli kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.