Wilaya ya Korogwe ni mojawapo kati ya wilaya 11 za Mkoa wa Tanga katika pwani ya Tanzania.

Mahali pa Wilaya ya Korogwe katika Tanzania (kijani cheusi).
Ramani ya mahali pa wilaya ya Korogwe katika mkoa wa Tanga

Mwaka 2002 ilikuwa na wakazi 261,004 [1]. Mnamo 2011 Wilaya ya Korogwe Mjini ilitengwa. Mwaka 2012 waliobaki upande wa vijijini walikuwa 242,038 walioishi katika kata 20 za wilaya. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 272,870 [2] katika tarafa 4, kata 29 na vijiji 118..

Makao makuu ya wilaya yako Korogwe mjini.

Kuna shule za msingi 118 na sekondari 27 na vituo vya afya 3.

Misimbo ya posta ya wilaya hii huanza kwa tarakimu 216[3].

Marejeo

hariri
  1. "Matokeo ya sensa 2002". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-03-18. Iliwekwa mnamo 2004-03-18.
  2. https://www.nbs.go.tz
  3. http://www.korogwedc.go.tz/

Viungo vya nje

hariri
  Kata za Wilaya ya Korogwe Vijijini - Mkoa wa Tanga - Tanzania  

Bungu | Chekelei | Dindira | Foroforo | Hale | Kalalani | Kerenge | Kizara | Kwagunda | Kwashemshi | Lewa | Lutindi | Magamba Kwalukonge | Magila Gereza | Magoma | Makumba | Makuyuni | Mashewa | Mazinde | Mgwashi | Mkalamo | Mkomazi | Mkumbara | Mlungui | Mnyuzi | Mombo | Mpale | Mswaha | Vugiri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Korogwe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.