Wilaya ya Kilindini

Wilaya ya Kilindini ilikuwa wilaya ya Mkoa wa Pwani wa Jamhuri ya Kenya. Makao makuu yake yalikuwa Mombasa mjini.

Shule ya Allidina Visram huko Mombasa, mnamo 2006, palikuwa mahali pa kituo cha Briteni cha "Kilindini" wakati wa Vita vya pili vya Dunia.

Mojawapo wa taasisi nyeti zilizokuwa zipatikana katika Wilaya ya Kilindini ni bandari ya Mombasa, kivuko kinachofanya safari zake kati ya Likoni na Kisiwa cha Mombasa.

Wilaya hiyo ilipewa jina lake kutokana na neno Bandari ya Kilindini na ndipo yalipokuwa makao makuu yake.