Wilaya ya Kisarawe
Wilaya ya Kisarawe ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Pwani yenye postikodi namba 61400.
Makao makuu ya wilaya yapo kwenye mji wa Kisarawe.
Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 95,614 [1]. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 159,226 [2].
Kabila la Wazaramo[3] ndilo kabila lenye watu wengi zaidi wilayani humo; watu wa kabila hilo husifika kwa uchangamfu wao na utayari wa kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kijamii, kisiasa na hata kiuchumi.
Shughuli mbalimbali za kilimo [4] hufanyika katika wilaya hiyo. Zao la mhogo hustawi sana katika majira yote ya mwaka.
Marejeo
hariri- ↑ [1]
- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ "Wazaramo: Kabila lenye sherehe lukuki, usipochangia, kushiriki unatengwa". Mwananchi (kwa Kiingereza). 2021-03-14. Iliwekwa mnamo 2024-06-04.
- ↑ "Maendeleo ya Kilimo na Maendeleo ya Vijijini | Tanzania | Countries & Regions | JICA". www.jica.go.jp. Iliwekwa mnamo 2024-06-04.
Kata za Wilaya ya Kisarawe - Mkoa wa Pwani - Tanzania | ||
---|---|---|
Boga | Chole | Kazimzumbwi | Kibuta | Kiluvya | Kisarawe | Kurui | Mafizi | Maneromango | Marui | Marumbo | Masaki | Msanga | Msimbu | Mzenga | Vihingo | Vikumburu |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Pwani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Kisarawe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |