Wilaya ya Muleba

Wilaya ya Muleba ni wilaya moja ya Mkoa wa Kagera, Tanzania yenye postikodi namba 35500 [1]. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 540,310[2].

Mahali pa Muleba (kijani) katika mkoa wa Kagera.

Muleba ilikuwa tarafa ya Bukoba ikaanzishwa kama wilaya ya pekee mwaka 1984. Makao makuu yako kwenye mji wa Muleba uliokuwa na wakazi 10,000 wakati wa sensa 2002.

Wilaya ina tarafa tano za Muleba, Kimwani, Nshamba, Izigo na Kamachumu. Eneo la wilaya ni kilomita za mraba 3,444 pamoja na 7925 km² za maji ya Ziwa Viktoria zikiwa pamoja na visiwa 20.

Marejeo

  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
  2. Sensa ya 2012, Kagera - Muleba-District-Council
  Kata za Wilaya ya Muleba - Mkoa wa Kagera - Tanzania
 

Biirabo | Bisheke | Buganguzi | Buhangaza | Bulyakashaju | Bumbire | Bureza | Burungura | Goziba | Gwanseli | Ibuga | Ijumbi | Ikondo | Ikuza | Izigo | Kabirizi | Kagoma | Kamachumu | Karambi | Kasharunga | Kashasha | Katoke | Kerebe | Kibanga | Kikuku | Kimwani | Kishanda | Kyebitembe | Mafumbo | Magata Karutanga | Mayondwe | Mazinga Kisiwa | Mubunda | Muhutwe | Muleba | Mushabago | Ngenge | Nshamba | Nyakabango | Nyakatanga | Ruhanga | Rulanda | Rutoro


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Muleba kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.