Kibanga ni kata ya Wilaya ya Muleba katika Mkoa wa Kagera, Tanzania, yenye postikodi namba 35515 [1].

Kijiji cha Kibanga kinapakana kaskazini na kijiji cha Kabare, kusini na mto Ngono, mashariki na kijiji cha Bumilo na magharibi na kijiji cha Kabutaigi.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 11,118 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 10,432 waishio humo.[3]

Wakazi wengi Kibanga ni wakulima na zao la biashara ni kahawa.

Kata ya Kibanga ina shule za msingi nne yaani: Kibanga, Bumilo, Runyinya na Kabutaigi. Kuna shule mbili za sekondari: moja ya binafsi inaitwa Dream Achiever Seconadary School, na nyingine ya serikali inaitwa Kibanga Secondary School.

Marejeo hariri

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01. 
  2. https://www.nbs.go.tz, uk 172
  3. Sensa ya 2012, Kagera - Muleba-District-Council
  Kata za Wilaya ya Muleba - Mkoa wa Kagera - Tanzania
 

Biirabo | Bisheke | Buganguzi | Buhangaza | Bulyakashaju | Bumbire | Bureza | Burungura | Goziba | Gwanseli | Ibuga | Ijumbi | Ikondo | Ikuza | Izigo | Kabirizi | Kagoma | Kamachumu | Karambi | Kasharunga | Kashasha | Katoke | Kerebe | Kibanga | Kikuku | Kimwani | Kishanda | Kyebitembe | Mafumbo | Magata Karutanga | Mayondwe | Mazinga | Mubunda | Muhutwe | Muleba | Mushabago | Ngenge | Nshamba | Nyakabango | Nyakatanga | Ruhanga | Rulanda | Rutoro


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kibanga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.