Willem Barents (au Barentsz, labda kutoka Barentzoon, mwana wa Barent; Terschelling, mnamo mwaka 1550 - 20 Juni 1597) alikuwa baharia na mpelelezi kutoka nchini Uholanzi.

Willem Barentsz

Barents anakumbukwa kama mgunduzi wa visiwa vya Spitsbergern (Svalbard). Alilenga kukuta njia ya kufika katika Bahari Pasifiki kupitia bahari ya Aktiki.

Bahari ya Barents [1] na mji wa Barentsburg vilipokea jina lake.

Marejeo

hariri