Witness Mwaijaga Sigbjorn

Witness Mwaijaga Sigbjorn (anafahamika kwa jina lake la kisanii kama Witnesz Kibonge Mwepec "au" kabla ya kuwa mshindi wa cocacola popstars alifahamika kama Bad Gear; amezaliwa 15 Novemba 1982) ni msanii wa hip hop na rapa kutoka nchini Tanzania.

Witnesz Kibonge Mwepec
Jina la kuzaliwa Witness Mwaijaga Sigbjorn
Pia anajulikana kama Witnesz Kibonge Mwepec
Amezaliwa 15 Novemba 1982 (1982-11-15) (umri 42)
Asili yake Dar es Salaam, Tanzania
Aina ya muziki Hip hop, rap
Kazi yake Rapa
Ala Sauti
Ame/Wameshirikiana na Fid Q, Langa Kileo, Sarah Kaisi, Mr. Abel Ochu Sheggy na wengine wengi wa ndani na nje ya Tanzania kama Marekani Norway na nchi zingine za kiafrica
Aliyekuwa msanii wa muziki nchini Tanzania

Anafahamika zaidi kwa kuwa mmoja kati ya washindi wa shindano la Coca Cola Pop Stars na mmoja wa wa wanzilishi wa kundi la muziki wa hip hop maarufu kama Wakilisha. Anavuma kwa baadhi ya vibao vyake kadhaa alivyofanya na kundi, pamoja na vya peke yake. Vibao hivyo ni pamoja na: Hoi, Kiswanglish, Kichekesho na [[Zero] n.k pia ana album yake inaitwa Khaya Khaya yenye nyimbo kumi, Iliyofanywa Tanzania na kuuzwa nchini Norway chini ya Lebo iitwayo Nedland Kultur

Witnesz kibonge Mwepec, alisoma katika Shule ya Msingi ya Oysterbay ya jijini Dar es Salaam, vilevile Shule ya Sekondari ya Jitegemee ambapo ndipo alipomazia. Pia, alishafanya kazi na mashirika ya kimataifa kama vile Unicef na alikuwa akifanya mikutano inayohusiana na masuala ya vijana.

Pia, alishawahi kuwa mcheza wa ngoma za asili na muziki wa asili yaani kuimba kwa kutumia ala za asili pia alikua ni muelimishaji rika wa ISHI, shirika la masuala ya mafunzo,uhamasishaji, Uelimishaji rika na maendeleo ya vijana Tanzania.

Viungo vya nje

hariri
  • Witness katika Tanzania Directoty.info
  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Witness Mwaijaga Sigbjorn kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.