Fid Q
Farid Kubanda (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Fid Q; amezaliwa katika hospitali ya Bugando iliyopo jijini Mwanza tarehe 13 Agosti 1980) ni msanii wa hip hop na Bongo Flava nchini Tanzania. Kabila lake ni msukuma.
Fareed Kubanda | |
---|---|
| |
Jina Kamili | {{{jina kamili}}} |
Jina la kisanii | Fid Q |
Nchi | Tanzania |
Alizaliwa | amezaliwa katika hospitali ya Bugando iliyopo jijini Mwanza tarehe 13 Agosti 1980 |
Aina ya muziki | Hip Hop |
Kazi yake | Msanii wa muziki wa Hip-hop nchini Tanzania |
Ameshirikiana na | Juma Nature Professor Jay Witness Ngwair Mr. Paul Daz Baba Langa Kileo Black Rhino T.I.D. Adiri Diamond Platnumz Rayvanny Fresh Lord Eyes Bi Kidude Young Killer |
Ala | Sauti |
Kampuni | Bongo Records Mj Records Baucha Records Cheusi Dawa[1] |
Maisha
haririFid Q alianza shughuli za muziki mnamo miaka ya 1990. Fid Q alitoa wimbo wake wa kwanza mwaka 2000 ulioitwa 'Huyu na Yule' ambao huo aliimba na msanii Mr Paul. wimbo huu ulimpa heshima kubwa, ulirekodiwa katika studio za MJ records chini ya usimamizi wake Master Jay mwenyewe.
Wimbo wake wa pili kutoka uliitwa 'Binti Malkia' ambao alimshirikisha Nuruelly. Ilivyofika mnamo mwaka wa 2004 Fid Q alivunja ukimya wake kwa wimbo wake mahiri uliokwenda kwa jina la "Fid Q.com", na wimbo huo aliufanya katika studio ya Baucha Records baada ya kuhama kwa MJ.
Wimbo huo uliirudisha ile hiphop ya Tanzania katika ramani yake halisi na inasemekana hivyo kwa sababu kipindi hicho ni kile ambacho wasaanii wengi wa muziki wa kufokafoka walikuwa wamejiingiza katika masuala ya uimbaji kwasababu kulikuwa na uvumi wa kwamba hip hop haikubaliki kwa watu wa Tanzania.
Fid anatajwa kuwa ni miongoni mwa wasanii walioleta heshima ya Hip hop Tanzania na Afrika mashariki na wimbo wake unaojulikana kama Mwanza Mwanza uliofanya vizuri ambapo ndani yake kuna uandishi wa kipekee ambao umeenda tofaut na ule uliokuwa umezoeleka(masimulizi/mipasho)
Mara kadhaa amekuwa akitajwa kama mwanahip hop bora wa muda wote Tanzania na Afrika mashariki (na Felix Nyaumbu).
Ilipofika 26 Januari ya mwaka 2008, Fid Q aliachia wimbo "Ni Hayo Tu" aliomshirikisha Prof. J na Langa. wimbo huo ulibahatika kujinyakulia Tuzo ya Kili ukiwa kama wimbo bora wa muziki wa hip hop kwa mwaka wa 2007-2008.
Tarehe 31 Desemba 2017, FidQ aliachia video ya wimbo Fresh Remix ambayo aliwashirikisha Diamond Platnumz na Rayvanny , Mpaka sasa Remix ya wimbo Fresh ndio video ya FidQ yenye watazamaji wengi kwenye mtandao wa YouTube ikiwa na watazamaji zaidi ya milioni 2.
Fid Q ana albamu tatu kwenye soko la muziki. Albamu ya kwanza inaitwa"Vina Mwanzo Kati na Mwisho". Mwishoni mwa mwaka 2009 alitoa albamu ya pili "PROPAGANDA", ambayo imepokelewa vizuri sana Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki. Mashabiki wa Hip Hop wanaichukulia PROPAGANDA kama ni albamu bora kabisa, yaani 'classic'. Ni kawaida kwa Fareed kuachia wimbo mmoja mpaka nyimbo mbili kila Agosti 13, Mwaka 2019 FidQ ameiachia Albamu yake ya tatu KitaaOLOJIA ambayo imesubiriwa kwa miaka mingi. KitaaOLOJIA ni Albamu yenye nyimbo 23 zikiwemo kolabo na Ay, TAZ, Ben Pol, Rosa Ree, Saida Karoli, waimbaji wa Injili Paul Clement, Melisa John na wengine wengi.
Fid Q ni kati ya wasanii wachache kutoka Afrika Mashariki ambao wanadumisha miiko muhimu ya Hip-Hop kama vile kuelimisha, grafiti, ucheguali na kuendeleza utamaduni. Katika wimbo wake Kiberiti aliomshirikisha msanii mkongwe Saida Karoli, Farid amechambua kitabu "The 4 Agreements" na kuelezea umihimu wa kutochukulia mambo kibinafsi kama njia moja ya kuvutia mafanikio na kuishi vizuri na watu. Zaidi ya umaarufu wake Fid Q ni mfuatiliaji mkubwa sana wa vitabu na kila anapozungumza na mashabiki wake huonekana mtu mwenye busara sana na uelewa mkubwa wa Hip-Hop na sanaa kwa ujumla. Ni msanii ambaye amewavutia vijana wengi Afrika Mashariki kufanya Hip-Hop na kuendeleza ushairi na mitindo huru. Anaamini kwamba rap ni kile unachofanya, Hip-Hop ni vile unavyoishi.
Albamu
haririFid Q ana albamu tatu kwenye soko la muziki. Albamu ya kwanza inaitwa"Vina Mwanzo Kati na Mwisho".[1] Mwishoni mwa mwaka 2009 alitoa albamu ya pili "PROPAGANDA", ambayo imepokelewa vizuri sana Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki. Mashabiki wa Hip Hop wanaichukulia PROPAGANDA kama ni albamu bora kabisa, yaani 'classic'. Ni kawaida kwa Fareed kuachia wimbo mmoja mpaka nyimbo mbili kila Agosti 13, Mwaka 2019 FidQ ameiachia Albamu yake ya tatu KitaaOLOJIA ambayo imesubiriwa kwa miaka mingi. KitaaOLOJIA ni Albamu yenye nyimbo 23 zikiwemo kolabo na Ay, TAZ, Ben Pol, Rosa Ree, Saida Karoli, waimbaji wa Injili Paul Clement, Melisa John na wengine wengi.
Marejeo
haririViungo vya nje
hariri- [Tovuti rasmi ya Fid Q Archived 12 Machi 2018 at the Wayback Machine.
Fareed Kubanda katika MySpace Fid Q - MistariYetu Archived 29 Septemba 2017 at the Wayback Machine. Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Fid Q kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
- Tovuti rasmi ya Fid Q Archived 12 Machi 2018 at the Wayback Machine.
- Fareed Kubanda katika MySpace
- Fid Q - MistariYetu Archived 29 Septemba 2017 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Fid Q kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |