Wolfgang Petersen (amezaliwa tar. 14 Machi 1941 mjini Emden, Lower Saxony, Ujerumani) ni mshindi wa Tuzo ya Academy, akiwa kama mwongozaji bora filamu wa Kijerumani. Anafahamika zaidi kwa kuongoza filamu ya kivita ya Das Boot ambayo ilimfanya ashinde Tuzo ya Academy mnamo mwaka wa 1982. Petersen pia ameongoza filamu nyingi tu zilizo maarafu kama vile Outbreak, In the Line of Fire, Air Force One, The Perfect Storm na Troy.

Wolfgang Petersen
Wolfgang Petersen wakati wa utengenezaji wa filamu ya Air Force One.
Wolfgang Petersen wakati wa utengenezaji wa filamu ya Air Force One.
Jina la kuzaliwa Wolfgang Petersen
Alizaliwa 14 Machi 1941
Ujerumani
Kazi yake Mwongozaji
Miaka ya kazi 1965 - hadi leo
Ndoa Ursula Sieg (kaach. 1978)
Maria Borgel-Petersen (1978-)

Wasifu

hariri

Maisha ya awali

hariri

Wolfgang Petersen alizaliwa wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mnamo tarehe 14 Machi katika mwaka wa 1941 katika kitongoji kidogo cha Emden-kaskazini mwa Ujerumani karibu kidogo na mpaka wa Dutch, mahali ambapo maji ya Mto Ems yanamwagikia katika Bahari ya Kaskazini. Kuanzia mwaka 1953 mpaka 1960 Petersen alihitimu eleimu yake ya msingi katika shule ya Johanneum ya mjini Hamburg.

Kunanko miaka ya 1960 alikuwa akiongoza tamthilia za Hamburg's Ernst Deutsch Theater. Baada ya kuhitimu masomo yake ya filamu katika chuo cha mjini Berlin na baadaye Hamburg, Petersen alimaliza rasmi elimu yake ya mambo ya filamu na televisheni katika cha chuo Berlin (1966–1970).

Filamu yake ya kwanza ilikuwa kwa ajili ya televisheni ya Kijerumani, na kazi zake zilikuwa katika kipindi kile cha mtindo maarufu wa Kijerumani uitwao Tatort ("Sinema za Uharifu") ambako huko aliongoza mfululuzo wa vipindi vya TV na alifanya kazi na Bw. Jürgen Prochnow — ambaye baadaye alimchukua na kwenda kucheza katika filamu ya Das Boot, ambapo humo alicheza kama Kapteni wa U-boat.

Filamu ziliongozwa na Wolfgang Petersen

hariri
  • Die Konsequenz (1977)
  • Das Boot (1981)
  • The NeverEnding Story (1984)
  • Enemy Mine (1985)
  • In the Line of Fire (1993)
  • Shattered (1991)
  • Outbreak (1995)
  • Red Corner (1997), as executive producer
  • Air Force One (1997)
  • The Perfect Storm (2000)
  • Troy (2004)
  • Poseidon (2006)
  • Ender's Game (2008)
  • Uprising (2008)

Marejeo

hariri
  1. Consequence, The (Konsequenz, Die) Archived 7 Desemba 2008 at the Wayback Machine.. PlanetOut.com.

Viungo vya nje

hariri