World Tofauti (Ulimwengu Tofauti) ni filamu ya Kikenya yenye maudhui ya mapenzi iliyo ongozwa na Kang'ethe Mungai. wahusika wakuu katika filamu iyo walikuwa ni Avril Nyambura na Innocent Njuguna pia Maureen Njau kama muhusika msaidizi.[1]

Kisa cha filamu hariri

Avril Nyambura aliye igiza kama (Nina) ni mwanamke aliyezaliwa na kukua katika makazi duni jijini Nairobi. Anakutana na Innocent Mungai aliye igiza kama (Hinga) mwanamume aliyetoka katika malezi bora pia akiwa na kazi nzuri, ambaye amekwama kwasababu ya tairi la gari kupasuka karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nina na genge lake wanamwibia Hinga vitu vyake vyote vya thamani. Kwa hali isiyo ya kawaida wawili hao wanazama katika penzi, wakati huo Hinga amemchumbia Maureen Njau aliye igiza kama (Ciru), ni mwenye nia ya kuongoza wanawake wenye historia sawa ya nyuma kijamii. Hinga anamsaidia Nina kufuatilia vitu vyake vya thamani na pia kukwepa mamlaka.[2]

Wahusika hariri

  • Avril Nyambura kama Nina, mwanamke aliye kulia katika mitaa duni jijini Nairobi, na kuishi maisha ya uhalifu.
  • Innocent Njuguna kama Hinga, mfanyabiashara mwenye mafanikio jijini Nairobi
  • Maureen Njau kama Ciru, mchumba wa Hinga anayedai na kudhibiti.

Kutolewa hariri

World Tofauti ilionyeshwa kwa mara ya kwanza katika Ukumbi wa Kitaifa wa Kenya jijini Nairobi, Tarehe 22 Desemba 2017.[3]

Marejeo hariri

  1. "ACTSCENE: Avril is a hustler in the movie ‘World Tofauti’". Nation (kwa Kiingereza). 2020-07-05. Iliwekwa mnamo 2022-08-08. 
  2. "actors.co.ke". actors.co.ke. Iliwekwa mnamo 2022-08-08. 
  3. "World Tofauti (@world_tofauti) on Instagram | Ghostarchive". ghostarchive.org. Iliwekwa mnamo 2022-08-08.