Yabezi Kiiza (20 Januari 19381 Agosti 2016) alikuwa mwanasiasa na mhandisi wa ujenzi wa Uganda. [1] Alihudumu kama Waziri Mkuu wa 13 wa Bunyoro, mojawapo ya falme za jadi za Uganda, chini ya Omukama Solomon Iguru I kuanzia mwaka 2009 hadi 2012.

Kiiza alikuwa mhandisi wa ujenzi. [2] Aliteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu wa Bunyoro mwaka wa 2007. Alikua Waziri Mkuu wa Ufalme huo mnamo Machi 2009 kufuatia kuondolewa kwa mtangulizi wake, Waziri Mkuu Emmanuel Aliba Kiiza.

Kiiza alijiuzulu nafasi ya Waziri Mkuu wa Bunyoro Januari 2012, kutokana na kuzorota kwa afya ikiwamo ugonjwa kisukari na shinikizo la damu. [3] [4] [5] Kiiza aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu tarehe 5 Januari 2012, na alistaafu mwishoni mwa Januari.

Yabezi Kiiza alifariki kutokana na matatizo ya kisukari na shinikizo la damu wakati wa matibabu Kituo cha Masindi Kitara huko Masindi tarehe 1 Agosti 2016, akiwa na umri wa miaka 78. [6]

Marejeleo hariri

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yabezi Kiiza kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.