Yaunde
Yaoundé ni mji mkuu na mji mkubwa wa pili nchini Kamerun baada ya Douala. Ina wakazi 1,299,369 (2021[1]
Jiji la Yaounde | |
Nchi | Kamerun |
---|
Jiografia
haririMji uko kwenye kimo cha 730 m juu ya UB katika vilima vya Kamerun ya magharibi takriban 160 km kutoka mwambao wa Atlantiki. Hali ya hewa ni ya kitropiki; halijoto ina wastani ya 23.3 C°. Mvua hunyesha Septemba / Oktoba na Aprili / Mei.
Historia
haririYaounde ilianzishwa mwaka 1888 BK na wanfanya biashara Wajerumani. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia na mgawanyo wa nchi ikawa sehemu ya Kamerun ya Kifaransa na mji mkuu wa koloni kuanzia mwaka 1922. Wakati wa uhuru mwaka 1961 ilikuwa mji kuu wa Kamerun yote pamoja na sehemu zilizokuwa chini ya Uingereza.
Uchumi
haririYaounde ni kitovu cha usafiri na mawasiliano ya nchi. Kuna viwanda vya tumbako, vyakula, vioo na ubao. Yaounde ni kitovu cha biashara kwa ajili ya kilimo cha kahawa, kakao, nguta na raba katika mazingira ya mji. Kuna pia migodi ya dhahabu na metali ya titani.
Waliozaliwa Yaounde
hariri- Roger Milla (20 Februari 1952) mchezaji mpira wa miguu
- Franck Songo'o (14 Mei 1987) mchezaji mpira wa miguu
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
hariri- Chuo Kikuu cha Yaounde Archived 24 Juni 2006 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Yaunde kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |