Yobes Ondieki
Yobes Ondieki (mzaliwa 21 Februari 1961 katika katika wilaya ya Kisii, Nyanza) ni mwanariadha wa 5000m wa zamani wa Kenya aliyeshinda mashindano ya dunia mjini Tokyo 1991. Katika mwaka huohuo aliweka rekodi isiyokaa ya mita 5000 ya kenya ya dakika 13.02.82 huko mjini Zürich. Alishiriki katika fainali za Olimpiki za miaka ya 1988 na 1992 lakini hakushinda medali.
Rekodi za medali | ||
---|---|---|
Men's Wanariadha | ||
Anawakilisha nchi Kenya | ||
World Championships | ||
Dhahabu | 1991 Tokyo | 5000 m |
Ondieki alijulikana kwa zoezi zake ngumu na uwezo wake wa kukimbia daima kwa mwendo wa kasi. Hata hivyo, alikosa nguvu za kutosha za kumaliza, udhaifu uliotumiwa na wapinzani wake kumshinda katika Olimpiki ya mwaka 1992 katika fainali ya 5,000 m hukoBarcelona. (Baadhi yenu mtakumbuka kuwa mwaka wa 1992 ulikuwa mara ya kwanza na ya pekee ambapo mtu mweupe (Dieter Baumann) alishinda fainali za mita 5000 katika Olimpiki tangu Said Aouita kushinda mwaka 1984.) Mwaka 1993, Ondieki alikuwa mwanariadha wa kwanza kuvunja kizuizi cha dakika 27 akikimbia mita 10000 katika michezo ya Bislett huko Oslo.
Ondieki alifunga ndoa na Lisa Martin, mwanariadha wa Australia. Mwaka 1990 walikuwa na mtoto msichana aitwaye Emma Ondieki. Sasa hivi, Ondieki na Martin wameachana.
Mnamo Septemba 1991 yeye na Martin walihudhuria AFL Grand Final ya mwaka wa 1991 kama sehemu ya burudani kabla ya michezo.
Marejeo
haririViungo vya nje
hariri- IAAF wasifu wa Yobes Ondieki
Records | ||
---|---|---|
Alitanguliwa na Richard Chelimo |
Men's 10,000 m World Record Holder 10 Julai 1993 – 22 Julai 1994 |
Akafuatiwa na William Sigei |
Sporting positions | ||
Alitanguliwa na John Ngugi |
Men's 5,000 m Best Year Performance 1989 |
Akafuatiwa na Salvatore Antibo |
Alitanguliwa na Salvatore Antibo |
Men's 5,000 m Best Year Performance 1991 |
Akafuatiwa na Moses Kiptanui |