Moses Kiptanui
Moses Kiptanui (amezaliwa 1 Oktoba 1970 katika Wilaya ya Marakwet, Kenya) ni mwanariadha wa mbio ya umbali wa wastani na refu.Anajulikana zaidi kwa mbio ya 3000m ya kuruka viunzi alipokuwa mwanariadha bora kabisa kati ya miaka ya 1991 hadi 1995 na ni bingwa wa IAAF mara tatu mfululizo. Kiptanui,pia, alikuwa mtu wa kwanza kukimbia mita 3000 kwa ,muda wa chini ya dakika nane.
Kiptanui aliyejitokeza katika mwaka wa 1991,alikuwa mwanariadha asiyejulikana sana. Yeye alishinda mbio kadhaa za Grand Prix katika msimu huo. Yeye alisherehekea ushindi mmoja kubwa mjini Zurich alipoanguka katika mkondo wa mwisho lakini bado akashinda kwa urahisi sana.
Ushindi wake katika mbio ya 1991 World Championships mjini Tokyo,hivyo basi haikuwashangaza wengi. Waangalizi wengi wa riadha waliudhika sana alipokosa kuchaguliwa kwa timu ya Kenya ya Olimpiki ya 1992 mjini Barcelona. Kiptanui alishindwa kuhitimu muda uliofaa katika mbio ya majaribio mjini Nairobi.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya Olimpiki,yeye aliweka rekodi mpya ya dunia ya mbio ya 3000 m mjini Cologne kwa muda wa 7:28.96 min. Siku tatu tu baadaye, yeye akavunja pia rekodi ya dunia ya 3000 m ya kuruka viunzi kwa muda wa 8:02.08 mjini Zürich. Mwaka uliofuata, yeye alionyesha ubingwa wake kwa mbio ya World Championship mjini Stuttgart. Yeye alishinda mbio ya 3000m ya kuruka viunzi katika 1994 IAAF World Cup [1]. [13]
Mwaka wa 1995, akavunja rekodi ya dunia 5000m huko Roma katika muda wa dakika 12:55.30 (8 Juni). Baada ya kushinda medali yake ya tatu ya World Championship huko Gothenburg na akweka rekodi mpya ya mbio ya 3000m ya kuruka viunzi kwa muda wa dakika 7:59.18 (16 Agosti).Akawa mtu wa kwanza duniani nzima kukimbia mbio hiyo chini ya dakika 8.
Mwaka mmoja baadaye, yeye alikosa medali ya dhahabu ya Olimpiki tena alipochukua nafasi ya pili katika fainali ya mbio hiyo katika Atlanta. Yeye alishindwa mwenzake,kutoka Kenya, Joseph Keter. Mwaka uliofuata,katika mbio za 1997 World Championship ya Athens,Ugiriki alishindwa kushinda medali yake ya dhahabu lakini akashinda ya fedha. Wilson Boit Kipketer ndiye alikuwa mshindi , mwanariadha kutoka Kenya.
Bado alikuwa akikimbia katika mwaka wa 2001 akilenga 2002 Commonwealth Games lakini hakushindana huko. Baada ya kustaafu, akawa kocha wa mbio. Katika mwaka wa 2008, yeye alikuwa kocha wa Ezekiel Kemboi aliyeshinda medali ya dhahabu ya Olimpiki. Yeye,pia,amekuwa mwenyekiti wa tawi la Wilaya ya Marakwet ya Athletics Kenya [16][2]. He has also been the chairman of the Marakwet District branch of Athletics Kenya [3].
Silas Kosgei,bingwa mtetezi wa vijana wa dunia katika mbio ya 3000m ya kuruka viunzi kutoka 2007: ni binamu yake.
Tuzo
hariri- 1990
- 1990 African Championships ya riadha - Cairo, Misri.
- 1500 m medali ya dhahabu
- 1990 IAAF World Junior Championships - Plovdiv, Bulgaria.
- 1500 m medali ya dhahabu
- 1990 African Championships ya riadha - Cairo, Misri.
- 1991
- 1991 World Championships ya riadha - Tokyo, Ujapani.
- 3000 m ya kuruka viunzi medali ya dhahabu
- 1991 All-Africa Games - Cairo, Egypt.
- 3000 m ya kuruka viunzi medali ya dhahabu
- 1991 World Championships ya riadha - Tokyo, Ujapani.
- 1993
- 1993 World Championships ya riadha - Stuttgart, Ujerumani.
- 3000 m ya kuruka viunzi gold medal
- 1993 World Championships ya riadha - Stuttgart, Ujerumani.
- 1994
- 1994 Goodwill Games - Saint Petersburg, Urusi.
- 5000 m medali ya dhahabu
- 1994 Goodwill Games - Saint Petersburg, Urusi.
- 1995
- 1995 World Championships ya riadha - Gothenburg, Uswidi.
- 3000 m ya kuruka viunzi medali ya dhahabu
- 1995 World Championships ya riadha - Gothenburg, Uswidi.
- 1996
- 1996 Summer Olympics - Atlanta, Marekani.
- 3000 m ya kuruka viunzi medali ya fedha
- 1996 Summer Olympics - Atlanta, Marekani.
- 1997
- 1997 World Championships in Athletics - Athens, Ugiriki.
- 3000 m kuruka viunzi medali ya fedha
- 1997 World Championships in Athletics - Athens, Ugiriki.
Marejeo
hariri- ↑ gbrathletics.com: IAAF WORLD CUP IN ATHLETICS
- ↑ The Washington Post, 31 Julai 2008
- ↑ Daily Nation, 5 Juni 2000: Polls open a new chapter in KAAA
Viungo vya nje
hariri- Moses Kiptanui Archived 24 Juni 2011 at the Wayback Machine.
Alitanguliwa na Said Aouita |
Mshindi wa mbio ya 3000m 16 Agosti 1992 — 2 Agosti 1994 |
Akafuatiwa na Noureddine Morceli |
Alitanguliwa na Haile Gebrselassie |
Mshindi wa 5000m 6 Juni 1995 – 16 Agosti 1995 |
Akafuatiwa na Haile Gebrselassie |
Alitanguliwa na Peter Koech |
Mshindi wa mbio ya 3000m ya kuruka viunzi 19 Agosti 1992 — 13 Agosti 1997 |
Akafuatiwa na Wilson Boit Kipketer |
Alitanguliwa na Dieter Baumann |
Mwanaume bora kabisa katika 3000m 1992 |
Akafuatiwa na Noureddine Morceli |
Alitanguliwa na Noureddine Morceli |
Mwanaume bora kwa mwaka katika 3000m 1995 |
Akafuatiwa na Daniel Komen |
Alitanguliwa na Yobes Ondieki |
Mwanaume bora kabisa katika mbio ya 5000 katika msimu huo 1992 |
Akafuatiwa na Ismael Kirui |
Alitanguliwa na Peter Koech |
Mwanaume bora kabisa katika 3000m 1991 – 1995 |
Akafuatiwa na John Kosgei |