Yuichi Kobayashi
Yuichi Kobayashi (小林 雄一, Kobayashi Yūichi, alizaliwa Itabashi, Tokyo, 25 Agosti 1989) ni mwanariadha nchini Japani ambaye alibobea mbio za mita 200. Aliwakilisha nchi yake katika mashindano ya dunia mara mbili mfululizo, mwaka 2011 na 2013.[1]
Mama yake Sumiko Kobayashi (née Kaibara) ni mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za mita 200 na upokezanaji vijiti wa mita 4 × 100 katika mashindano ya Asia mwaka 1979 huko Tokyo.[2] Pia alikuwa mshikilizi wa zamani wa rekodi ya Kijapani katika mita 200 kwa muda wa sekunde 24.27.[3]
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yuichi Kobayashi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |