Yussuf Yurary Poulsen (alizaliwa 15 Juni 1994) ni mchezaji wa soka wa Denmark mwenye asili ya Tanzania ambaye anacheza katika klabu ya Ujerumani iitwayo RB Leipzig kama mshambuliaji au winga.

Yussuf Poulsen (2016)

Kazi ya klabu

hariri

RB Leipzig

hariri

Mafanikio yake yalivutia sana vilabu vingi vya kigeni na hata ndani ya nchi, na tarehe 3 Julai 2013, alisaini mkataba na klabu ya ujerumani iitwayo RB Leipzig. Alimaliza msimu wa 2013-14 na kufunga magoli 10 katika mechi 27.

Yussuf alipanda katika ligi ya Bundesliga mwaka 2014 na mwaka 2016 alikuwa amefunga magoli 12 katika mechi 32 wakati wa msimu wa 2014-15 akifunga magoli saba katika mechi ambazo alicheza ni 32 wakati wa 2015 -16 msimu.

Mechi ya 6 ya msimu wa 2016-17, alifunga goli lake la kwanza la Bundesliga kwa ushindi wa 2-1 nyumbani dhidi ya FC Augsburg. Alimaliza msimu wa 2016-17 na magoli matano katika mechi 30 alizocheza.

  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yussuf Poulsen kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.