Zain Verjee

mtangazaji wa runinga

Zain Verjee (alizaliwa 11 Februari 1974) ni mwandishi wa Kanada mwenye asili ya Kihindi aliyezaliwa na kulelewa nchini Kenya. Hivi sasa ni mtangazaji wa habari katika kipindi cha CNN cha World Report yaani ripoti ya dunia nzima, kipindi hiki huandaliwa jijini London,Uingereza. Hapo awali, yeye alifanya kazi kama msoma habari katika kipindi cha The Situation Room, mwanahabari mshirika wa idara ya serikali na mtangazaji mwenza wa kipindi cha CNN cha Your World Today.

Jumba la habari la CNN,Atlanta

Verjee alijiunga na CNN katika mwaka wa 2000, kabla ya hayo alikuwa msomaji wa habari katika Mfumo wa Runinga wa Ghana,jijini Nairobi. Ameripoti habari mbalimbali na matukio ya duni nzima:mkutano wa Waziri Mkuu Atal Bihari Vajpayee wa India na Rais Pervez Musharraf wa Pakistan, migogoro ya Mashariki ya Kati,kesi ya aliyekuwa kiongozi wa Yugoslavia(Slobobdan Milosevic), mashambulizi ya 11 Septemba,Hajj na vita nchini Iraq. Yeye ,pia,huripoti kuhusu habari ya biashara barani Afrika katika kipindi cha kila wiki cha Inside Africa katika stesheni ya CNN.Kipindi hiki huhusu habari ya kindani na kamilifu ya bara la Afrika.

Mnamo Julai 2006, aliripoti kutoka kwa DMZ ya Korea na katika mwezi wa Septemba, aliko fanya mahojiano na aliyekuwa rais wa Iran, Mohammed Khatami.

Zain ni Mwislamu wa Ismaili. Katika mawazo yake kuhusu Safari ya Mecca, yeye aliandika:

"Kuna msemo wunaosema kuwa muumini anayesafiri kuenda Mecca kwa Hajj anafaa kutoka jiji hilo takatifu ili asiipende sana."

Alichapisha hivi majuzi kitabu Live & On the Air, kitabu cha watoto kinachochunguza maisha ya msichana kutoka vijiji anahamia Nairobi kutafuta kazi kama mtangazaji wa habari. Verjee amezalisha pia kampeni zilizofanikiwa za kusambaza ujumbe kuhusu Ukimwi, Hepatitis B na Polio.

Mnamo 16 Januari 2008,alipokuwa akirekodi ripoti kuhusu maandamano ya kupinga serikali mjini Nairobi,aligongwa mgongoni kwa mkebe mwenye gesi ya machozi uliotupwa na polisi.Video hiyo ilionyeshwa baadaye katika stesheni ya CNN.Hakuumia sana katika tukio hilo.

Masomo hariri

Marejeo hariri

  1. https://web.archive.org/web/20050909042700/http://cnnstudentnews.cnn.com/CNN/anchors_reporters/images/verjee.zain.jpg
  2. http://www.cnn.com/2008/WORLD/africa/01/16/kenya.tension/index.html

Viungo vya nje hariri