Zap Mama
Zap Mama ni kundi la muziki la Ubelgiji lililoanzishwa na kuongozwa na mwanamke Marie Daulne. Daulne alisema mpango wake ni kuwa daraja baina ya watu wa Ulaya na Afrika na kuzileta tamaduni zote mbili pamoja kwa kutumia muziki wake.[1] "Kitu nilichokuwa ninapenda kukifanya ni kuleta midundo ya Kiafrika na kuipeleka katika dunia ya Kimagharibi, kwa sababu naamini kupitia muziki na midundo yake, watu watagundua tamaduni mpya, watu wapya na dunia mpya," alisema Marie.
Zap Mama hupiga muziki mchanganyiko ikiwemo miziki ya Kiafrika, R&B, na Hip-hop na kuzielekezea sauti katika namna ya muziki wao wanavyoupiga.
"Sauti huwa zinafanya midundo zenyewe," alisema Daulne. "Ni midundo asilia. Misingi ya midundo. Midundo ya kupendezesha nafsi, sauti ya wanadamu.
"Zap Mama huwa wanaimba kwa lugha ya Kifaransa, ya Kiingereza na za Kiafrika zaidi, hasa Kiswahili.
Albamu za muziki
haririDiscography
hariri- Zap Mama (1991)
- Adventures in Afropea (1993)
- Sabsylma (1994)
- Seven (1997)
- A Ma Zone (1999)
- Ancestry in Progress (2004)
- Supermoon (2007)
- ReCreation (2009)
- Eclectic Breath (2018)
Zap Mama pia walishiriki katika kutengeneza kibwagizo cha filamu za Mission Impossible 2 na Iko-Iko (1999).
Marejeo
haririViungo vya nje
hariri- Tovuti rasmi ya Zap Mama Ilihifadhiwa 4 Julai 2008 kwenye Wayback Machine.
- Tovuti ya mashabiki wa Zap Mama Ilihifadhiwa 9 Agosti 2018 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Zap Mama kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |