Ziwa Duluti ni kati ya maziwa madogo ya Tanzania. Linapatikana katika mkoa wa Arusha kwenye barabara kati ya Moshi na Arusha katika mji mdogo wa Tengeru.

Mandhari ya ziwa Duluti

Uso wa ziwa unapatikana kwenye kimo cha mita 1290 juu ya UB; eneo la maji ni Km² 0.6. Kina chake ni takriban mita 9. Hupokea maji yake kutoka chemchemi chini yake na kupoteza maji kwa njia ya uvukizaji, maana hakuna mito inayoingia wala kutoka[1]

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri