Moshi (mji)
Moshi ni makao makuu ya Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania.
Mji wa Moshi | |
Mahali pa mji wa Moshi katika Tanzania |
|
Majiranukta: 3°20′24″S 37°20′24″E / 3.34000°S 37.34000°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Kilimanjaro |
Wilaya | Moshi Mjini |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 221,733 |
Wakazi
haririKwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, mji huo una wakazi wapatao 184,292. Katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 331,733 [1].
Kabila linaloongoza kwa idadi ya wakazi wa mji wa Moshi ni Wachagga wakifuatiwa na Wapare na makabila mengine yaliyohamia kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania kama Wasambaa, Warangi n.k. Wachagga wanapenda vyakula vinavyopikwa kwa kutumia ndizi kama vile mtori, kitawa, na machalari.
Wakazi wengi wa Moshi ni wakulima, wafugaji na wafanyabiashara. Watu wengi wanakwenda Moshi kufanya kazi na kurudi nyumbani jioni.
Ukuaji wa mji wa Moshi hauendani na mipango halisi ya 'Mipango Miji'. Hii inatokana na kutokufuatiliwa kwa sheria mbalimbali zinazohusu uendelezaji wa miji.
Hali ya hewa
haririMoshi ni mji wenye baridi katika miezi ya Juni mpaka Agosti na joto katika miezi ya Oktoba hadi katikati ya Januari.
Utalii
haririMji wa Moshi una mandhari nzuri ya kuvutia watalii. Watalii hupenda sana mji wa Moshi kwa sababu ya mlima Kilimanjaro na huduma muhimu kama mahoteli na usafiri.
Kampuni nyingi za utalii zimekuwa zikiendesha shughuli zake miaka na miaka. Shughuli kuu za utalii zikiwa ni kupanda mlima Kilimanjaro na kwenda mbuga za wanyama kama vile Serengeti, Ngorongoro, Tarangire na Ziwa Manyara.
Elimu
haririMji wa Moshi una vyuo vikuu vinne:
- MUCCoBS (Moshi University College Of Cooperative and Business Studies) ambacho ni chuo kikuu kishiriki cha Sokoine University of Agriculture (SUA) ya Morogoro
- MWUCE (Mwenge University College Of Education) ambacho ni chuo kikuu kishiriki cha SAUT (St. Augustine University - Mwanza)
- KCMC Medical School chini ya Chuo Kikuu cha Tumaini
- OUT (The Open University of Tanzania) ambacho ni tawi la chuo chenye jina hilohilo chenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam
Utawala
haririKiutawala mji wa Moshi ni wilaya ya Mkoa wa Kilimanjaro. Ndani yake kuna kata 15 ambazo ni Bondeni, Kaloleni, Karanga, Kiboroloni, Kiusa, Korongoni, Longuo, Majengo, Mawenzi, Mji Mpya, Msaranga, Njoro, Pasua, Rau na Kilimanjaro.
Marejeo
haririRamani | Wilaya au manisipaa | Wakazi (2022) | Tarafa | Kata | Kijiji | Eneo km² |
---|---|---|---|---|---|---|
Wilaya ya Hai | 240,999 | 17 | 1,217 | |||
Wilaya ya Moshi Vijijini | 535,803 | 32 | 1,300 | |||
Wilaya ya Moshi Mjini | 331,733 | 21 | 63 | |||
Wilaya ya Mwanga | 148,763 | 20 | 1,831 | |||
Wilaya ya Rombo | 275,314 | 28 | 1,471 | |||
Wilaya ya Same | 300,303 | 34 | 6,221 | |||
Wilaya ya Siha | 139,019 | 17 | 1,217 | |||
Jumla | 1,861,934 | 152 | 13,209 | |||
Wilaya ya Siha hii ilianzishwa mwaka 2007 kutokana na maeneo ya wilaya ya Hai. | ||||||
Marejeo: Mkoa wa Kilimanjaro |
Kata za Wilaya ya Moshi Mjini - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania | ||
---|---|---|
Bomambuzi | Bondeni | Kaloleni | Karanga | Kiborloni | Kilimanjaro | Kiusa | Korongoni | Longuo B | Majengo | Mawenzi | Mfumuni | Miembeni | Mji Mpya | Msaranga | Ng'ambo | Njoro | Pasua | Rau | Shirimatunda | Soweto |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Moshi (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|