Zulia
Zulia ni aina ya kitambaa kinene ambacho mara nyingi hutumiwa kufunika sakafu.
Mazulia hutumiwa kwa madhumuni mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuhami miguu ya mtu kutoka kwenye ubaridi wa sakafu ya saruji, kufanya chumba kuwa kizuri zaidi kama mahali pa kukaa sakafu (kwa mfano, wakati wa kucheza na watoto au kama mahali pa sala), kupunguza sauti ya kutembea (hasa katika majengo ya ghorofa) na kuongeza mapambo au rangi kwenye chumba. Mazulia hutengenezwa kwa rangi yoyote kwa kutumia nyuzi tofauti za rangi. Kuanzia miaka ya 2000, mazulia yanatumiwa pia katika viwanda, maduka ya rejareja na hoteli.
Inaaminiwa kuwa mazulia yalianza kutumika karne ya 3 au 2 KK huko Asia ya Magharibi, labda eneo la Bahari ya Kaspi (Irani ya kaskazini) au Miinuko ya Armenia. Zulia zee kabisa duniani ni zulia la Pazyryk[1] ambalo ni la karne ya 5 KK. Zulia hili lilifukuliwa na Sergei Ivanovich Rudenko mwaka wa 1949 kutoka kwenye milima Altai huko Siberia.
Marejeo
hariri- ↑ "The State Hermitage Museum: Collection Highlights". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-10-05. Iliwekwa mnamo 2017-11-07.
Tazama pia
haririViungo vya Nje
hariri- Je ni nani aliyegundua mazulia?
- Historia ya mazulia
- Kuhusu zulia na sala
- Jinsi Waislamu wanavyotumia mazulia kwenye sala Archived 13 Oktoba 2017 at the Wayback Machine.
- Kuhusu zulia na sala
- Ushauri wa jinsi ya kutunza mazulia
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Zulia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |