İpek Emiroğlu
İpek Emiroğlu (alizaliwa Denizli, 1992) ni mwamuzi wa mpira wa miguu wa chama cha wanawake nchini Uturuki.[1]
Maisha ya awali
haririİpek Emiroğlu ni mwanafunzi wa udaktari wa mifugo katika Chuo Kikuu cha Uludağ huko Bursa.
Kazi ya uamuzi
haririEmiroğlu alianza kazi ya urefa katika mechi ya Ligi ya Wanaume chini ya miaka 21 mnamo 2009. Alichezesha mechi kadhaa za Ligi za wanaume kama vile Regional Amateur League,TFF Third League na katika ngazi zote za ligi za wanawake kama mwamuzi msaidizi. Alichezesha kwa mara ya kwanza kama mwamuzi katika mechi ya Ligi ya wanawake daraja la pili mnamo Desemba 1, 2013, na pia kwa mara ya kwanza kama mwamuzi katika Ligi ya Wanawake ya daraja la kwanza mnamo Novemba 9, 2014.[2][3]
İpek Emiroğlu ndiye mwamuzi wa mpira wa miguu mwanamke mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kutokea nchini Uturuki.
Marejeo
hariri- ↑ "İPEK EMİROĞLU - Referee Details TFF". www.tff.org. Iliwekwa mnamo 2023-04-03.
- ↑ "İPEK EMİROĞLU - Referee Details TFF". www.tff.org. Iliwekwa mnamo 2023-04-03.
- ↑ "NİYE KLASMAN DÜŞTÜLER?". www.hakeminsesi.com.tr. Iliwekwa mnamo 2023-04-03.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu İpek Emiroğlu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |