Msimu wa Kwanza wa mfululizo wa kipindi cha televisheni cha 24 ulianza kurushwa hewani mnamo tar. 6 Novemba 2001 hadi 21 Mei 2002. Mwanzo wa hadithi ya msimu huu inaanzia saa 6:00 usiku katika siku ya uchaguzi wa Rais wa Marekani.

Msimu wa 1 wa 24

Washiriki wa Msimu wa 1
Nchi asilia Marekani
Mtandao Kampuni ya Utangazaji ya Fox
Iko hewani tangu Novemba 6, 2001 (2001-11-06) – Mei 21, 2002 (2002-05-21)
Idadi ya sehemu 24
Tarehe ya kutolewa DVD 17 Septemba 2002 (toleo halisia); 20 Mei 2008 (toleo maalum) (NTSC, Widescreen)
Msimu ujao Msimu wa 2
Sasa hivi, magaidi wanapanga njama za kumwua mgombea urais. Mke wangu na binti yangu wametekwanyala... na watu ninaofanyanao kazi huenda wakawa wanahusika wote. Mimi ni Kachero wa FBI Jack Bauer, na leo ni siku ndefu sana katika maisha yangu.

Muhtasari wa Msimu hariri

Msimu wa Kwanza (2001 – 2002) umechukua nafasi wakati wa uchaguzi mkuu wa rais wa Marekani wa mwaka wa 2001 (kimaigizo).

Njama kuu za msimu huu ni jaribio la kutaka kumwua Seneta wa Maryland Mh. David Palmer, mgombea urais mteule wa chama cha demokrasia, katika siku ya uchaguzi wa rais huko California. Mhusika wa kati ni Jack Bauer, kiongozi wa zamani wa Delta Force ambaye baadaye akawa Mkurugenzi wa Kitengo cha Kuzuia Ugaidi cha Los Angelese (CTU).

Bauer amekuwa mtaalamu zaidi pale watu waliohusika na masuala jaribio la uuaji kushirikisha pia maisha binafsi kwa kuitekanyala familia yake, mke wake Teri na Kim.

Umuhimu wa msimu umegawanyika katika vifungu viwili:

  1. Kifungu cha kwanza kinahusisha kikundi cha watu waliokodiwa kufanya juhudi ya kumdhibiti Jack Bauer na kumlazimisha kumwua Seneta Palmer kwa kumtekanyala mke wake na binti yake Bauer. Hii iliashia kwa Jack kufaulu kuiokoa familia yake.
  2. Kifungu cha pili, muhusika mkuu wa njama zote akajulikana na akawa anaendeleza mpango wa kumwua Seneta na familia ya Bauer vilevile.

Marejeo hariri

Viungo vya Nje hariri