A Good Man is Hard to Find

A Good Man Is Hard to Find and Other Stories ni mkusanyo wa Hadithi Fupi za mhariri wa Marekani Flannery O'Connor. Kitabu hichoi kilichapishwa nchini Uingereza kwa jina Artificial Nigger and Other Tales. Mkusanyiko huu ulichapishwa mara ya kwanza mnamo 1955. Vichwa vya hadithi zilizomo vinagusia maswala ya Ubatizo ("The River") na hata wauaji wa muda mrefu ("A Good Man Is Hard to Find"), ulafi wa kibinadamu na unyanyasaji ("The Life You Save May Be Your Own").

A Good Man is Hard to Find  
Mwandishi (wa){{{mwandishi}}}
NchiUnited States
LughaEnglish
MchapishajiHarcourt, Brace and Company
ISBNISBN:

Yaliyomo

hariri

Kitabu hiki kina shirikisha hadithi zifuatazo:

Kichwa

hariri

Kichwa cha hadithi ya O'Connor kilichukuliwa kutoka kwa wimbo wa mwenendo wa blues"A Good Man Is Hard to Find," uliotungwa na Eddie Green na kuimbwa na Bessie Smith mnamo1927.

Nyimbo zenye vichwa vinavyohusiana

hariri

Bendi ya Morphine imetoa wimbo kwa jina "A Good Woman Is Hard to Find" katika albamu yao ya "The Night".

"A Good Man Is Hard to Find" pia ni Kichwa cha kibao cha mwisho katika albamu ya 002 ya Tom Waits ya Blood Money.

Bruce Springsteen alitoa wimbo uitwao "A Good Man Is Hard to Find (Pittsburgh)" mnamo 1998 katika albamu yake ya mwaka huo Tracks. Springteen ametaja kuwa usomaji wake wa maana ulianza na wahariri kama O'Connor, ambaye kazi yake anahisi ilinasa maswala ya Marekani ambayo alikuwa anatamani kuyaangazia katika kazi yake.[1] Archived 26 Novemba 2009 at the Wayback Machine.

Sufjan Stevens ana wimbo "A Good Man Is Hard to Find" katika albamu yake Seven Swans; hadithi yake ikisimuliwa na mwasi, ingawa yeye mwenyewe si lengo la wimbo huo.

Matoleo ya Kifilamu, TV na Jukwaani

hariri

Igizo la Televisheni la hadithi "The Life You Save May Be Your Own," likimshirikisha Gene Kelly kama nyota, lilikuwa kipindi cha televisheni ya CBS network Schlitz Playhouse mnamo 1 Februari 1957. O'Connor hakupendezwa na matokeo."[1]

Muundo wa kifilamu wa hadithi ya "A Good Man Is Hard to Find", ambao uliitwa "Black Hearts Bleed Red", ulitengenezwa mnamo 1992 na mtengeneza filamu wa New York Jeri Cain Rossi. Filamu hii inashirikisha msanii mashhughuli wa New York Joe Coleman [2]

Igizo la jukwaani la dakika 45 linalitokana na "A Good Man Is Hard to Find" lilikamilishwa mnamo 2003 na David Volk, mmoja wa wanafunzi wa muziki katika chuo cha Georgia kama mradiwake wa mahitaji katika utunzi wa kisanaa. Igizo hili lilifanyiwa Seney-Stovall Chapel jijini Athens kwa msaada wa kifedha kutoka kwa chuo kikuu cha Ideas for Creative Exploration (ICE). Baadaye mwaka huo, kazi yake iliigizwa tena katika chuo cha Piedmont jijini Demorest, GA, na pia Milledgeville, GA, "Flannery O'Connor: The Visionary and the Venacular," ambalo ni kongamano la nyanja mbalimbali lililothaminiwa na chuo cha Georgia (ambacho pia ni maskani ya Flannery O'Connor Library). Mnamo 2007, kazi hii iliigizwa katika tawi la Chuo Kikuu cha Virginia mjini Wise ambapo Dk. Volk anafunza kama Profesa msaidizi wa Somo la Muziki.

Tanbihi

hariri
  1. Fitzgerald, Sally. Flannery O'Connor: The Habit of Being. Vintage. ku. 191, 205.

Viungo vya Nje

hariri