Adili na nduguze ni riwaya ya Shaaban Robert inayozungumzia jinsi ambavyo Adili, kijana mwenye roho na tabia njema, alihusudiwa na ndugu zake (Hasidi na Mwivu), walimchukia na kumpatia mateso na kumweka katika hali ngumu katika nyakati tofauti.

Hao walimtesa kiasi cha kutosha na kama malipo ya makosa yao wakageuzwa manyani na jini liitwalo Huria. Lakini kwa moyo wake mwema Adili akayaombea msamaha baada ya miaka mingi yakitunzwa naye kwa mateso ya kuyapiga kiboko kila usiku na kuyapa posho.

Baada ya hapo Huria alikubali pendekezo la Adili wakarejea katika utu tena. Mara baada ya baba yao kufariki dunia Adili na nduguze waligawana mali sawa kwa sawa katika sehemu tatu.

Kwa sehemu Kubwa kitabu cha Adili na Nduguze kimefanana na kitabu cha kwanza cha Alfu Lela U Lela.

Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Adili na Nduguze kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.