Admerali (pia: admeri, admirali) ni cheo cha kiongozi mkuu wa kijeshi wa wanamaji. Cheo hicho kinalingana na jenerali katika matawi mengine ya jeshi.

Kola, bega, na nembo ya alama kwa Admiral katika Jeshi la Wanamaji la Merika

Neno linatokana na Kiarabu أمير البحر amir-al-bahr yaani "mwenye mamlaka baharini". Iliingia katika lugha za Ulaya kama "admiral".

Cheo hicho si kawaida katika jeshi la majini la Tanzania wala Kenya, lakini hutumiwa kutafsiri vyeo vya kigeni[1].

Marejeo

hariri
  1. Linganisha "Admeri", katika Kamusi Kuu ya Kiswahili, Longhorn - Bakita 2016, ISBN 9789987020984