Ajali (kutoka neno la Kiarabu; kwa Kiingereza: "accident" au "uninentional injury") ni tukio maalumu linalotambulika na lisilotarajiwa, geni na lisilotakikana ambalo hutokea katika muda na mahali fulani bila sababu au makusudi dhahiri, lakini husababisha madhara yaliyo wazi, hasa vifo.

Kitalu cha benchi chaanguka katika mashindano ya soka ya vyuo ya Big12, kikiwabwaga mashabiki.

Ajali hudokeza kwa ujumla matokeo mabaya ambayo labda yangeweza kuepukwa au kukingwa ikiwa matukio yaliyosababisha ajali hiyo yangetambuliwa na kurekebishwa kabla ya tukio hilo.

Wataalamu katika nyanja za kuepuka majeraha hawatumii neno 'ajali' kuelezea matukio ambayo husababisha majeraha katika jaribio la kubainisha asili ya majeraha mengi ambayo yangeweza kukingwa. Matukio kama hayo huzingatiwa kutoka mtazamo wa epidemiolojia - yanaweza kuepukwa na kukingwa. Maneno yanayopendelewa huweza kulifananua tukio lenyewe zaidi, badala ya asili yake isiyotakikana (k.m kugongana, kufa maji, kuanguka, n.k)

Ajali ya aina ya kawaida (magari, moto, n.k.) huchunguzwa ili kubaini jinsi ya kuepukana nazo katika siku zijazo. Mara nyingine hii hujulikana kama uchambuzi wa sababu ya asili, lakini haihusu ajali ambazo haziwezi kutabiriwa. Sababu haswa ya ajali ya nadra isiyoweza kuepukwa huenda ikawa haiwezi tambulika, na hivyo matukio ya siku zijazo yatabaki kuwa "ajali."

Ufafanuzi

hariri

Unapofafanua kinaganaga, ajali huweza kutaja tukio lenyewe pekee, bila kuzingatia mazingira ya tukio hilo, au athari za tukio hilo, yaani "ajali" huishia katika tukio la mara moja, ambalo huleta athari ambazo hazikutarajiwa.

Hata hivyo, katika matumizi ya kawaida, 'ajali' huenda ni pamoja na mfumo mzima wa mazingira (fursa, iliyokuwepo awali, au matokeo yanayojiendeleza bila kuthibitishwa; matokeo ya kawaida; wakati na mahali yasiyoweza kutabiriwa; washiriki n.k.) yanayoelekea, pamoja na kusababishwa na tukio hilo.

 
Vifo kutokana na ajali nchi kwa nchi mwaka 2012
     107-247     248-287     288-338     339-387     388-436     437-505     506-574     575-655     656-834     835-1,165

Kimaungo na yasiyo ya kimaungo

hariri

Mifano ya kimaungo ni kama migongano isiyotarajiwa au maanguko, kujeruhiwa kwa kugusa kitu kikali, moto, au umeme, au kunywa sumu.

Mifano ya ajali isiyo ya kimaungo ni kama kutoboa siri bila kutaka au kusema kitu kimakosa, kusahau miadi, n.k.

Katika shughuli

hariri
  • Ajali wakati wa utekelezaji wa kazi huitwa ajali kazini.
  • Kwa kulinganisha, ajali zinazotupata tukibarizi au tunapostarehe huwa sanasana ni majeraha ya michezo.

Kwa vyombo vya usafiri

hariri

Tunatakiwa tuendeshe vyombo vya usafiri kwa uangalifu ili kupunguza ajali, kama vile:

Sababu za kawaida

hariri
 
Matukio ya ajali, yakibainishwa kwa shughuli.

Kwa majeraha ya kimwili yanayopeleka watu kulazwa hospitalini, nyingi huwa ni ajali za barabarani na kuanguka.

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: