Chombo cha usafiri

(Elekezwa kutoka Vyombo vya usafiri)

Chombo cha usafiri ni kifaa chochote kinachotumiwa kusafirisha watu au mizigo.

Basi ni chombo maarufu cha usafiri duniani

Vyombo vya usafiri hutofautiana kama vinahudumia usafiri wa nchi kavu, wa majini au wa hewani.

Mifano ni

Hutofautishwa pia kama vinalenga matumizi ya watu binafsi au matumizi ya umma.

  • Baisikeli, pikipiki na motokaa mara nyingi hutumiwa na wenye chombo hiki cha usafiri. Lakini zinaweza kutumiwa pia kama sehemu ya usafiri wa umma kwa mfano gari kama teksi au baisikeli kama boda-boda. Magari makubwa na mazito kama lori husafirisha mizigo.
  • Treni, reli ya mjini, metro na mabasi ni vyombo vya usafiri wa umma kwenye nchi kavu.
  • Meli na feri ni vyombo vya usafiri wa umma majini, lakini boti ndogo mara nyingi hutumiwa na watu binafsi. Isipokuwa kuna miji kando ya mto au bandarini penye huduma ya teksi ya maji kwa kutumia boti dogo. Meli ya mizigo husafirisha bidhaa.
  • Eropleni ndogo hutumiwa na watu binafsi ilhali matajiri wachache ni wenye ndege kubwa. Kwa kawaida ndege kubwa hubeba abiria kama vyombo vya usafiri wa umma. Eropleni ndogo zinapatikana pia kama teksi ya hewani.