Al Capone
Al Capone (kwa jina halisi Alphonse Gabriel Capone; 17 Januari 1899 - 25 Januari 1947) alikuwa mhalifu mashuhuri nchini Marekani. Alizaliwa jijini New York katika ukoo wa wahamiaji kutoka Italia akahamia Chicago ambako aliongoza genge la uhalifu katika enzi ya prohibition ambako pombe ilipigwa marufuku Marekani.
Capone alisimamia sehemu kubwa ya biashara haramu ya pombe pamoja na ukahaba mjini Chicago, Illinois, kuanzia mwaka 1925 hadi 1931. Genge lake lilishambulia wenye vilabu vya siri waliokataa kununua pombe kutoka kwake na kupigana na magenge mengine, ambako watu waliuawa.
Hatimaye vyombo vya dola vilifaulu kumpeleka mahakamani kwa mashtaka ya ukwepaji wa ushuru wa mapato. Alipatikana na hatia, Capone alihukumiwa kifungo cha miaka 11 gerezani.
Capone aliachiliwa kutoka gerezani mnamo 1939 kwa sababu alikuwa mgonjwa akaaga dunia mnamo 1947 baada ya kupata kiharusi. [1]
Tanbihi
hariri- ↑ "Capone Dead At 48. Dry Era Gang Chief", New York Times, 2009-04-02. Retrieved on 2010-03-12. Archived from the original on 28 January 2010. "Al Capone, ex-Chicago gangster and prohibition era crime leader, died in his home here tonight."
Marejeo
hariri- 2.“Al Capone.” World of Criminal Justice. Gale, (2002). Biography in Context.Web. 10-June 2014
Viungo vya nje
hariri- Tovuti ya Mario Gomes kwenye kila kitu kinachohusiana na Al Capone
- Jarida la South Beach Mgeni Ambaye Hajakaribishwa: Al Capone huko Miami. (na picha)
- Kamilisha faili za FBI kwenye Al Capone
- Little Chicago: Capone katika Johnson City, Tennessee Ilihifadhiwa 1 Desemba 2006 kwenye Wayback Machine. Archived
- Al Capone kwenye Maktaba ya Uhalifu
- Works by or about Al Capone