Alan Dugan
Alan Dugan (12 Februari 1923 – 3 Septemba 2003) alikuwa mshairi kutoka nchi ya Marekani. Mwaka wa 1962 alipokea Tuzo ya Pulitzer ya Ushairi.
Kitabu chake cha kwanza kilichapishwa mwaka 1961 na kushinda kama mshairi kijana.
Kitabu chake cha mwisho kiliitwa kwa jina la Poems Seven: New and Complete Poetry, kilichapishwa mwaka 2001 na Seven Stories Press kutoka New York City anakilishinda tena kwa mara ya pili tuzo za National Book Award
Maisha
haririDugan alikulia nchini Jamaica, na kupigana vita vya pili vya dunia ambapo alijifunza pia ushairi lakini kabla ya hapo hakuwa mtu wa kupendelea mashairi.
Aliishi katika jimbo la Massachusetts, ambapo alikuwa mwanachama wa katika kituo cha Fine Arts Work Center.
Alan Dugan alimuoa mwanasanaa Judith Shahn, na alifariki kwa ugonjwa wa pneumonia mnamo Septemba 3, 2003, akiwa na umri wa miaka 80.[1]
Tuzo
haririKatika maisha yake Dugan alipata tuzo zifuatazo
- Mshairi kijana katika tuzo za National Book Award for Poetry 1962
- Complete Poetry mwaka 2001 National Book Award.[2]
- Tuzo ya Prix De Rome ilotolewa na National Institute of Arts and Letters mwaka 1962
- Tuzo ya The Shelley Memorial Award olotolewa na Poetry Society of America mwaka 1982
- Tuzo katika fasihi ilotolewa na American Academy and Institute of Arts and Letters mwaka 1985
- Tuzo ya Lannan Literary Awards ya mwaka 2002.
Kazi zake
hariri- Poems (1961)
- Poems 2 (1963)
- Poems 3 (1967)
- Poems 4 (1974)
- Poems Five: New and Collected Poems (1983)
- Poems Six (1989)
- Poems Seven: New and Complete Poetry (2001)
Marejeo
hariri- ↑ https://www.nytimes.com/2003/09/05/arts/alan-dugan-80-barbed-poet-of-daily-life-s-profundities.html New York Times Obituary
- ↑ "National Book Awards – 2001". National Book Foundation. Retrieved 2012-03-03.
Viungo vya Nje
haririMakala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Alan Dugan kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |