Ali Muhsin al-Barwani
Ali Muhsin Al-Barwani (13 Januari 1919 katika Mji Mkongwe - 20 Machi 2006 katika mji mkuu wa Muskat (Omani)) alikuwa mwanasiasa, mwanadiplomasia, na mshairi kutoka nchi ya Zanzibar chini ya Usultani wa Zanzibar. Alikuwa Waziri wa mambo ya nje wakati wa mamlaka ya Kiarabu baada ya Zanzibar kupata uhuru kutoka kwa mkoloni Muingereza na kabla ya Zanzibar kugeuka kuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
Wasifu
haririMaisha ya Sheikh
haririSheikh Ali Muhsin Al-Barwani alikua mzalendo wa nchi ya Zanzibar ambae alipata mafunzo ya dini kwa baba yake Sheikh Muhsin bin Ali na kwa wanazuoni wengine pia wa Afrika ya Mashariki. Pia Sheikh Ali amesoma ilimu ya Kilimo Chuo Kikuu cha Makerere (Makerere University) huko Uganda.
Sheikh Ali alianza maisha yake kwa kufanya kazi ya kilimo na uwalimu. Katika mwaka 1947 Aliacha kazi ya serikali, ili ashughulikie jihadi ya nchi yake na Umma wake.
Kazi yake ya magazeti
haririSheikh Ali alikua Mhariri Mkuu wa gazeti la Mwongozi kwa muda wa miaka kumi na tano. Mwongozi lilikua gazeti la siasa na jamii na la dini, na lilikua maarufu gazeti hilo kwa kazi yake kubwa ya kudai haki za wananchi na kutapakaza misingi ya Kiislamu huko Zanzibar na sehemu mbali mbali za Afrika ya Mashariki
Kuongoza kwake Chama cha Hizbu
haririSheikh Ali Muhsin aliongoza chama cha Hizbu(Zanzibar Nationalist Party) na aliongoza jihadi ya Uhuru wa Zanzibar dhidi ya Muingereza. Hapo aliitwa Zaim na raia wa Zanzibar yaani zaim ni Kiongozi.
Kazi zake
haririSheikh Ali alitumika kazi mbali mbali huko Zanzibar alifanya kazi ya Waziri wa Ilimu na Waziri wa Mambo ya ndani, Baadae akapewa kazi ya Naibu wa Waziri mkuu, na Waziri wa Mambo ya nje katika serikali ya Kidemokrasia ya Zanzibar.
Serikali yake kupinduliwa
haririJanuari mwaka 1964, serikali yake ilipinduliwa mapinduzi hayo yalisababisha kumwagika kwa damu za watu wengi hadi ulimwengu ulishtuka kutokana na kumwagika damu hizo maana walikufa watu wengi sana, Sheikh Ali Muhsin aliwekwa jela kwa zaidi ya myaka kumi bila kushtakiwa kwa sababu ya fikra zake za kisiasa.
Kuachwa kwake
haririMwaka 1974 Sheikh Ali Muhsin alifunguliwa nakuachiwa huru, akaamua kuondoka nakuelekea Kenya nakuomba ukimbizi na wakati alipopata ukimbizi aliamua kuelekea Misri, Kairo, Alikaa muda mrefu huko Kairokiasi cha myaka 10 na huko alisoma katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar nchini Misri, yeye alikua rafiki mzuri wa raisi wa Misri Gamal Abdel Nasser. Baada ya kukaa muda mrefu huko Misri aliamua kurejea Kenya, na baadae aliamua kuelekea Falme za Kiarabu,Dubai na huko huko ndio alifasiri Qurani kwa Lugha ya Kiswahili ambayo inaumashuhuri mwingi kwa wale Waislamu wazungumzao Lugha ya Kiswahili ulimwenguni haswa Afrika ya Mashariki na ya Kati pia na ya Kusini na Visiwa vya bahari Hindi
Tungo zake kadhaa
haririAmetunga Mashairi ya Kiswahili yenye beti 1300 Juu ya maisha ya mtume Muhammad (S.A.W) Ametunga kitabu cha Kiingereza cha Kulinganisha Ukristo na Uiislamu alikifasiri mwenyewe kwa lugha ya Kiswahili pia. Amefasiri Qurani tukufu kwa Lugha ya Kiswahili.("Al Muntakhab Fi Tafseer Al Qur'an".)
Kufa kwake
haririSheikh Ali Muhsin (Mungu amuweke mahala pema) aliiaga dunia siku ya Jumatatu mwezi wa Machi,2006, Alifariki akiwa na umri wa myaka 86.
Viungo vya nje
hariri- Kuhusu Sheikh kwa kirefu katika Coastweek Ilihifadhiwa 14 Septemba 2008 kwenye Wayback Machine.Kiingereza
- Kuhusu Sheikh katika Tovuti mashuhuri ya Mwambao
- Kurani kwa Lugha ya Kiswahili Ilihifadhiwa 22 Desemba 2021 kwenye Wayback Machine.