Alma Redemptoris Mater

"Alma Redemptoris Mater" (tamka: ˈalma redempˈtoris ˈmater; maana yake: 'Mpendwa Mama wa Mkombozi') ni utenzi wa Kikristo unaotumika katika liturujia ya Kanisa la Kilatini hasa kama antifona mojawapo ya kumalizia Sala ya mwisho nje ya Kipindi cha Pasaka.

Madonna kadiri ya Raffaello Sanzio.
Alma Redemptoris Mater kwa muziki wa fahari.

Utenzi huo ulitungwa na Hermannus Contractus (1013–1054) kwa kutegemea maandishi ya Fulgensyo wa Ruspe, Epifani wa Salamina na Irenei wa Lyon.[1].

Maneno asili kwa Kilatini

hariri

Alma Redemptóris Mater, quæ pérvia cæli
Porta manes, et stella maris, succúrre cadénti,
Súrgere qui curat pópulo: tu quæ genuísti,
Natúra miránte, tuum sanctum Genitórem
Virgo prius ac postérius, Gabriélis ab ore
Sumens illud Ave, peccatórum miserére.

[2]

Tafsiri huru ya Kiswahili

hariri

Ewe Mama wa Kristo, sikia kilio chetu,
Ewe nyota ya bahari, ewe Mlango wa mbingu,
Mama wa yeye mwenyewe, ambaye alikuumba,
Tunapozama topeni, msaada twakuomba;
Kwa furaha ile ile, Gabrieli alokupa,
E Bikira wa pekee, wa kwanza na mwisho pia,
Twakuomba utujalie, tupewe yako huruma.

[3]

Muziki wake

hariri

Utenzi huo ulipambwa kwa muziki na Marc-Antoine Charpentier.

Tanbihi

hariri
  1. : The Tradition of Catholic Prayer by Christian Raab, Harry Hagan 2007 ISBN 0-8146-3184-3 page 234
  2. Handbook of Prayers by James Socías 2006 ISBN|0-87973-579-1 page 472
  3. "Sala ya Kanisa", BPNP, uk. 1236.